ad

ad

KANYE WEST AMTAKA KIM ABADILI JINA

NEW YORK, MAREKANI
RAPA Kanye West amemtaka Kim Kardashian aliye mjamzito kubadili jina lake kuwa Kim West mara watakapo anza michakato ya kufunga pingu za maisha.
Kwa mujibu wajarida la Star, si tu kwamba Kardashian amekubali kuchukua jina la mwisho la rapa huyo, bali atataka pia mtoto wao mtarajiwa kuwa na jina hilo!
Lakini, chanzo cha jarida hilo kimedai kuwa, “Kim alimwambia Kanye kwamba daima atabaki kuwa Kardashian,hatakama atachukua jina hilo, kauli iliyomfadhaisha rapa huyo, lakini Kim aligoma kuifuta.
“Pia Kim anadhani hiyo ni njia ya kumfanya Kanye ajue kwamba hayuko nae kwasababu ya fedha zake,” kilidai chanzo hicho.
Powered by Blogger.