ad

ad

Kocha Yanga aiota Azam..“Naamini uwezo wa timu yangu, ila hata wapinzani wetu ni wazuri

KOCHA Mkuu wa vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, Ernie Brandts amesema mechi ijayo dhidi ya Azam FC, inamnyima usingizi kutokana na kiwango na nafasi waliyonayo wapinzani hao kwenye mbio za kuwania ubingwa.
 
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Brandts alisema licha ya timu yake kuwa imara kwa sasa, anahofia mechi hiyo ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

“Naamini uwezo wa timu yangu, ila hata wapinzani wetu ni wazuri. Ndiyo maana naifikiria sana hiyo mechi japokuwa ni ya kawaida kama nyingine, tatizo kubwa ni nafasi ambayo tunagombania nao, tunawazidi pointi tatu tu,” alisema Brandts.
Brandts alisema mbali ya kuiwazia mechi hiyo, atapigana kufa na kupona ili mwakani timu yake iweze kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa kama ilivyo Simba kwa mwaka huu.

“Naumia sana kuona timu yangu haishiriki katika michuano hii ambayo ni moja ya nafasi ya kuwapeleka nje ya nchi wachezaji, najitahidi nitakavyoweza mwakani lazima tushiriki na sisi,” alisema Brandts.

Naye Ofisa habari wa klabu hiyo, Baraka Kazuguto alisema kikosi chao jana kilikuwa kwenye mapumziko, na leo kitaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Yanga ndio vinara wa ligi hiyo kwa pointi 36; ikifuatiwa na Azam yenye pointi 33, huku Simba ambao ni mabingwa watetezi, wakiwa nafasi ya tatu kwa pointi 28.
Powered by Blogger.