Katibu Mkuu wa (TFF), Angetile Osiah ataja kinachoiua Simba
Na George Kayala
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limewaangushia lawama nzito aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic na Patrick Liewig kwa kushindwa kuwa na mabeki wa uhakika.

Katibu
Mkuu wa (TFF), Angetile Osiah amesema kuwa tangu msimu wa Ligi Kuu Bara
uanze, Simba ikiwa chini ya Milovan haina mabeki wa kati wa kueleweka
na ndicho kinachochangia kufanya vibaya kwa timu yao.
“Simba tangu kuanza msimu huu mabeki wake wa katikati hawachezi kwa kuelewana. Kila mchezo inaocheza huwezi kujua Shomari Kapombe atapangwa na nani au Juma Said ‘Nyosso’, hali hiyo imesababisha kufanya vibaya katika michezo yake,” alisema Osiah.
Katibu huyo alisema kuwa tatizo hilo limeendelezwa na Mfaransa, Liewig ambaye naye ameshindwa kujua awasimamishe mabeki gani katikati ambao ndiyo roho ya timu.
Akizungumzia mchezo wa marudiano kati ya Simba na Recreativo do Libolo wiki mbili zijazo, Osiah alisema kuwa vijana hao wa Msimbazi wanaweza kutinga hatua ya pili endapo watacheza kama timu.

Post a Comment