ad

ad

Matumizi mabaya ya dawa za binadamu

Kwa muda sasa nimekuwa nikisikia matumizi ya dawa za binadamu kwa wanyama na ndege. Katika pita pita zangu kwenye duka la dawa baridi leo nimabaini ukweli.
Anaingia dada mmoja na kuuliza:
" kuna tetracyline."
Muuza dawa:"hakuna"
Dada:"Hivi zinapakina kweli?"
Muuza dawa:"kwa shida, watu wachache sana wanazinunua"
Dada:"Mi mwenyewe nazitafuta kwa ajili ya kuku wangu."
Nilikuwa pembeni nikugana na kumueleza kuwa hizo dawa zimetengenezwa kwa ajili ya binadamu na anaweza kupata dawa za kuku kwenye maduka ya wanyama.


Tetracycline ni antibiotic inayotumika kutibu bacteria wa aina tofauti. Dawa hii imechangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa ugonjwa wa kipindupindu na pia hutumika kutibu chunusi na trachoma.
Tanzania ni mojawapo ya nchi ambayo matumizi mabaya ya madawa yameelezwa kuwepo.
Zimekuwepo habari za matumizi ya dawa za kupunguza makali ya ukimwi kwa kuku pamoja na nguruwe.Pia imeripotiwa matumizi ya vidonge vya majira na antibiotics nyingine kwenye kuku. Dawa hizi zimekuwa zikitumiwa na wafugaji kutibu magonjwa ama kukuza haraka mifugo yao.
 Hii ni hatari kwani ni mojawapo ya vitu vilivyochangia  kuibuka kwa usugu wa dawa. Sababu nyingine ni kuuzwa dawa bila cheti cha daktari, kutokumaliza dozi ama kutofuata taratibu za kutumia dawa.

Nchini Afrika Kusini imeripotiwa matumizi ya dawa za kukata makali ya ukimwi kuchanganya na dawa za kulevya. Na matumizi ya namna hii yanatokwa katika nchi mbalimbali.

WHO imetoa taarifa ya kuwa nchi za Afrika mashariki zimekumbwa na tatizo la Usugu wa antibiotics kwa kiasi kikubwa. Tatizo hili husababisha kuongezeka kwa gharama za afya ikiwemo kuhatarisha uhai.
Nini kifanyike
Serikali lazima ichukue hatua za ziada Mosi, kuimarisha huduma za kilimo mijini na vijijini. Dawa za mifugo zipatikane kwa urahisi na kwa bei nafuu.
Pili, usajili wa mabanda ya mifugo kwa serikali za mitaa.
Tatu,ukaguzi wa mabanda ya kufugia ili kufanya utambuzi wa kemikali zinazotumiwa na wafugaji. Hii iambatane na adhabu kali kwa wale watakaobainika kutumia dawa za binadamu.
Nne, ukaguzi wa maduka ya dawa baridi uimarishwe ikiwemo maduka kutakiwa kuonesha vyeti vya dawa zilizouzwa.
Kama tukitilia msisitizo mambo hayo tutaokoa afya za  watanzania wengi.

No comments

Powered by Blogger.