JOSE MOURINHO AIZUNGUMZIA MANCHESTER UNITED: “Tunajua tunaweza kuwafunga. Tunajua wanaweza kutufunga
JOSE
MOURINHO ameupamba mpambano wa Ligi ya Mabingwa kati ya Real Madrid na
Manchester United kama “mechi ambayo dunia inataka kuiona.”
Kocha
huyo wa Real alikuwapo Old Trafford Jumapili akiipeleleza United wakati
ikicheza na Liverpool, kuelekea mechi yao itakayopigwa Februari 13 –
ikiwa ya kwanza katika hatua ya mtoano ya timu 16.
“Hii ni mechi ambayo dunia inataka kuiona. Real Madrid dhidiya Manchester United.Sir Alex dhidi ya rafiki yake Mourinho.
“Ubaya pekee ni kwamba si mechi ya fainali,” alisema Mourinho aliye maarufu kwa jina la Special One.
Mourinho,
anayepigana kuiwezesha Real kubeba taji la kumi katika michuano hiyo,
aliongeza: “Tunajua tunaweza kuwafunga. Tunajua wanaweza kutufunga —
lakini tutakuwa tayari.”
Mreno
huyo hata hivyo anaamini kuwa Madrid inayoongozwa na staa wa zamani wa
United, Cristiano Ronaldo, iko vizuri zaidi baada ya kufuzu hatua hiii
kitokea ‘Kundi la Kifo’.
“Kulikuwa na makundi ambayo ulijua yupi atakwenda kuwa wa kwanza na wa pili baada ya mechi mbili au tatu.
“Lakini
kundi letu lilijumuisha timu tatu kati ya tano bora katika mashindano —
Borussia Dortmund, Manchester City na sisi. Sasa tumepata mpinzani
mgumu katika mechi kubwa ya timu 16 za mwisho,” alifafanua.
Post a Comment