Je raia wa Afrika Kusini wanashangazwa na ubakaji?
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa bado
anaishi katika chumba kimoja katika mtaa wa mabanda wa Soweti wakati
polisi walipokuja kumkamata siku chache kabla ya mkesha wa siku kuu ya
mwaka mpya.
Kwa mujibu wa mashahidi kadhaa, mtu huyo alikuwa
amembaka msichana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na saba katika baa
moja, na alihisi kuwa kitendo hicho ni cha kawaida na hivyo hakujaribu
kutoroka.
Hamna hata mtu mmoja katika baa hiyo, mbali na msichana huyo alifikiria kupasha polisi habari kuhusiana na tukio hilo.
Wakati ambapo taifa la India, linachunguza
sheria za nchi hiyo kufuatia tukio la ubakaji, Afrika Kusini inaonekana
kuwa imezembea.
Serikali ya nchi hiyo imeonekana kutojali yale
yanayotendeka licha ya takwimu kubainisha viwango vya ubakaji nchini
humo viko juu hata kuliko taifa la India.
Vijana katika eneo la Soweto
Visa elfu sitini vya ubakaji huripotiwa kila
mwaka nchini Afrika Kusini, idadi ambayo ni maradufu ya visa
vinavyoripotiwa nchini India.
Lakini wataalamu wanahisi kuwa visa hivyo huenda
vikawa vingi zaidi kwa kuwa mara nyingi wasichana wanaobakwa huwa
hwajitokezi kutoa habari kwa polisi.
Mapema wiki hii vyombo vya haabri nchini Afrika
Kusini, vilichapisha habari kuhusu kile kinachosemekana kuwa mtindo
mpya, ambao wanawake wakongwe ndio wanaolengwa na wabakaji.
Nyingi ya visa hivyo hulenga kina mama walio na umri mkubwa katika maeneo mashambani.
Katika matukio haya wamama wawili walio na umri wa miaka 82 na 73 walibakwa tarehe mbili mwezi huu.
Licha ya hasira na ghadhabu iliyojitokeza
miongoni mwa raia wa nchi hiyo ambao walipiga simu katika vituo vya
radio, viongozi wa taifa hilo bado hawajaona umuhimu wa kukabiliana na
janaga hilo.
Katika siku za hivi karibu, waandishi wa habari
na wanaharakati wa kijamii, wamekuwa wakichunguza matukio yanayoendelea
nchini India, huku wakiwa na matumaini kuwa yangelitendeka nchini humo,
kwa kuwa kujadili suala hilo pekee halitoshi.
Kuna idadi kubwa ya wabakaji Afrika Kusini
Mpumelelo Mkhabela Mhariri wa gazeti moja la Soweto
Mhariri mkuu wa gazeti la Mpumelelo Mkhabela, la
Soweto, Mpumelelo Mkhabela, amesema kuna haki ya raia wa nchi hiyo
kujitokeza zaidi na kupambana na tatizo la ubakaji.
Mkhabela, kwa upande mmoja anasema serikali ya
nchi hiyo imejitahidi, lakini raia nao wanapaswa kujitolea na kuchangia
katika harakati hizo, badala ya kuonyesha ghadhabu kwa siku moja.
Kwa sasa inakisiwa kuwa Afrika Kusini, ndilo
taifa linaloongozwa kwa visa vya ghasia na ubakaji barani Afrika na
duniani kwa ujumla.
Visa vya ubakaji vimekuwa vikiendelea kwa kwa miongo kadhaa na raia wengi wanayaona kama ni matukio ya kawaida.
Katika jamii nyingi nchini humo, kina mama
huzungumzia jinsi wanavyotarajia kudhalalishwa huku wavulana nao
wakiishi huku wakiwa na dhana kuwa wao wana haki zaidi kuliko wasichana
na kina mama.
Lakini mapema wiki hii, raia wa nchi hiyo
walighadhabishwa sana na tukio la kubakwa kwa msichana mmoja, mwenye
umri wa miaka 21, na kundi moja la vijana, tukio ambao ambalo
limeangaziwa pakubwa na vyombo vya habari nchini humo.
Wasichana na wamama wanaishi kwa wasiwasi
Msichana mmoja katika mtaa wa Soweto
Msichana huyo alibakwa akiwa njiani kwenda kujisajili katika chuo kimoja kikuu nje ya mji wa Pretoria.
'' Kwa sasa hatuko salama hata kidogo, kila siku tunahofia kuwa unaweza kubakwa'' Alisema msichana mmoja katika chuo hicho.
Ripoti zinasema msichana huyo alikamatwa na watu wanne ambao walimvuta hadi kichakani ambako walianza kumbaka.
Kwa bahati nzuri msichana huyo alinusurika.
Wanafunzi wengi katika chuo hicho ambao hawakuwa wamesikia tukio hilo, hawakushangzwa.
Wengi wao walikuwa wakiendelea na shughuli zao za kupiga foleni ili kutafuta nafasi ya kusoma licha ya jua kali..
Mwanamme mmoja ambaye alikuwa akipita hapo alikiri kuwa kuna idadi kubwa ya wabakaji katika eneo hilo.
Kwa mshangao mama mmoja ambaye alikuwa miongoni
mwa waliokuwa wakipiga foleni, aligeuka huku akiwa na hasira, na kusema
'' Sijui ni nini mbaya na wanaume wa siku hizi''.
'' Ni lazima jambo la dharuru lifanyike ili kukabiliana na matukio ya ubakaji'' alisema msichana huyo.

Post a Comment