Tevez kusaini mkataba mpya-Mancini
Kocha
wa Manchester City, Roberto Mancini, asema anatarajia kuwa mazungumzo
kuhusu kandarasi ya nyota wake Carloz Tevez yataanza hivi karibuni.
Tevez, mwenyi umri wa miaka 28, alijiunga na
Manchester City mwaka wa 2009 na nusura mchezaji huyo akihame klabu hiyo
pale Mancini aliposhutumu kwa kutokubali kuingia uwanjani kama mchezaji
wa ziada, kabla ya kurejea nyumbani kwao Argentina.
Hata
hivyo mzozo huo ulitatuliwa na Tevez alirejea tena na kuisadia
Manchester City, Kushinda kombe la ligi kuu ya Premier mwaka uliopita,
kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1968.,
Mkataba wake na klabu hiyo inatarajiwa
kukamilika mwaka wa 2014 na Mancini amesema ana matarajio makubwa kuwa
mchezaji huyo kutoka Argentina atasaini kandarasi mpya.
Kwingineko, Liverpool, imesitisha kandarasi ya mchezaji wake Nuri Sahin, ambaye alikuwa akiicheza kwa mkopo.
Sahin sasa ataichezea klabu ya Borussia Dortsmund kwa muda wa miezi kumi na nane ijayo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alijoiunga
na Liverpool, Agosti mwaka uliopita, kutoka klabu ya Real Madrid na
alitarajiwa kuicheza Liverpool msimu huu.
Lakini baada ya kuichezea mechi kumi na mbili
pekee na kufunga magoli matatu pekee, kocha wa Liverpool, Brendan
Roggers ameamua kusitisha kandarasi ya mchezaji huyo.
Mchezaji huyo kutoka Uturuki, alianza kucheza
soka ya kulipwa na klabu ya Dortmund na mwaka wa 2011, aliisaidia klabu
hiyo kushinda ligi kuu ya Ujerumani na pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora
wa mwaka, mwaka wa 2010.

Post a Comment