ad

ad

CAPITAL ONE CUP: CHELSEA 0 vs SWANSEA 2. MICHU NA GRAHAM

Makosa mawili ya Branislav Ivanovic leo kwenye CAPITAL ONE CUP yaimeifungisha timu yake ya Chelesea goli zote mbili na kwa makosa mawili ya  kizembe.
Dakika ya 39 kipindi cha kwanza Branislav Ivanovic amefanya makosa ya kupokea mpira kutoka kwa kipa na kutoutoa haraka na hatimaye mpira kuupata mshambuliaji wa Swansea Michu na hatimaye kuipachikia timu yake goli la kwanza.
Na dakika ya 90 kwenye dakika za nyongeza za lala salama Branislav Ivanovic  ametoa pasi hewa kwa nyuma na kutomfikia kipa na hatimaye Danny Graham kuupata na kumfunga kipa Ross Turnbull wa Chelsea.

Michu akitupia kwenye nyavu goli la kwanza dakika ya 39 kipindi cha kwanza.
Michu akishangilia kwa aina yake
Swansea wameweza kuwakaba kisawa sawa Chelsea leo usiku
hupiti hapa....
Ivanovic akikabwa na mchezaji wa Swansea
Danny Graham akimfunga Ross Turnbull goli la pili dakika ya 90+2 baada ya Ivanovic kufanya kosa.
Danny Graham slots home Swansea's second goal
...Nyavu...Ivanovic nguvu zikimwishia ...
Torres kafulia leo..
Shabiki aliyekosa kuvumilia kuona Chelsea inafungwa 2-0 Darajani na Swansea na kuingia uwanjani na hapa akiondolewa nje na askari.

VIKOSI:
CHELSEA: Turnbull, Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Cole, Luiz, Ramires (Lampard 71), Hazard, Oscar (Marin 83), Mata, Torres (Ba 81).
 Subs: Hilario, Ferreira, Bertrand, Ake.
SWANSEA: Tremmel, Rangel, Chico, Williams, Davies, Britton, De Guzman, Ki, Routledge (Tiendalli 63), Hernandez, Michu (Graham 84).
Subs: Vorm, Dyer, Monk, Shechter, Agustien.

Goal: Michu 39, Graham 90
Referee: Anthony Taylor


RATIBA/ MATOKEO-NUSU FAINALI
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku]
Jumanne Januari 8
Bradford 3 v Aston Villa 1
Jumatano Januari 9
Chelsea 0 v Swansea City 2
 

MARUDIANO
Jumanne Januari 22
Aston Villa v Bradford
Jumatano Januari 23
Swansea City v Chelsea

FAINALI
Jumapili Februari 24
Uwanja wa Wembley, London 

Powered by Blogger.