Sandro Tonali: Nyota wa Newcastle Anayevutia Klabu Kubwa
Manchester United imeanza rasmi harakati za kuimarisha kikosi chake kwa msimu ujao baada ya kuibuka taarifa kwamba kiungo mahiri wa Newcastle United, Sandro Tonali, yupo juu kabisa kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa majira ya joto.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Uingereza, United wanatafuta mbadala wa muda mrefu wa eneo la kiungo huku Casemiro akitarajiwa kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu, na Tonali ameonekana kuwa chaguo sahihi kutokana na uwezo wake wa kucheza kama kiungo mkabaji na mpangaji wa mashambulizi
Tonali, aliyesajiliwa na Newcastle akitokea AC Milan mwaka 2023 kwa ada ya takribani pauni milioni 55, sasa thamani yake imepanda hadi karibu pauni milioni 80–100, jambo linalomaanisha klabu itakayemtaka italazimika kuvunja benki
Klabu Kubwa Zaanza Kuvutana
Si Manchester United pekee wanaomuwania nyota huyo wa Italia.
Taarifa zinaeleza kuwa Arsenal, Chelsea na Manchester City pia zimeonyesha nia ya kumsajili, huku baadhi ya vigogo wa Serie A kama Juventus wakitajwa kufuatilia kwa karibu hali yake. Hii inaashiria kuwa dirisha la usajili linaweza kushuhudia vita kali ya dau
Hali ya Tonali Newcastle
Wakati tetesi zikizidi kupamba moto, inaelezwa kuwa Tonali ameanza kuonyesha dalili za kutoridhishwa na mwenendo wa Newcastle, hasa baada ya matokeo yasiyoridhisha ya hivi karibuni. Hata hivyo, mchezaji huyo bado ana mkataba na klabu na anaendelea kutimiza majukumu yake kitaalamu
Wakala wake pia amedokeza kuwa maamuzi kuhusu mustakabali wake yatajadiliwa zaidi mara tu msimu utakapomalizika.
Man United Wajipanga upya
Kwa upande wa Manchester United, huu unaonekana kuwa mwanzo wa mapinduzi mapya ya kikosi, huku benchi la ufundi likilenga kuleta damu changa na wachezaji wenye nguvu katikati ya uwanja.
Iwapo dili hili litakamilika, Tonali anaweza kuwa moja ya usajili mkubwa zaidi wa majira ya joto na kuongeza makali makubwa katika safu ya kiungo ya Mashetani Wekundu.

Post a Comment