Kiredio Aibua Maswali Kuhusu Ma-Ex: “Wanaachana Kinyonge Sana Siku Hizi!” Valentine Diary Yaendelea
Maudhui na mtayarishaji wa content za mitandaoni, Vicent Njau maarufu Kiredio, ameendelea kuwapa burudani mashabiki wake kupitia mfululizo wa Valentine Diary, lakini safari hii ameibua mjadala mzito kidogo tena kwa utani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kiredio aliandika kwa mzaha:
“Hivi hawa wako serious au ndio content ya Valentine? 😀😀
Ma Ex gani wanaachana halafu husikii hata wakichambana?
Ifike mahali hata tuone interview ya mmoja basi akimsema vibaya mwenzake.
Wanaachaanaje kinyonge hivyo 😀”
Kauli hiyo imewachekesha wengi mitandaoni, huku baadhi wakisema siku hizi mahusiano yanaisha kimya kimya bila drama kama zamani.
Kiredio aliendelea kuongeza utani kwa kuandika:
“Nimeulizwa Nile au Nioge Kwanza? @pwalles1
Sema nini 😂 Niombeeni tu leo
Dodoma mmeniweza 🙌🙌🙌
This is Valentine Diary Page No.10”
Chapisho hilo linaonekana kuwa sehemu ya mfululizo wake wa Valentine Diary, unaoangazia visa vya mapenzi, vichekesho na matukio ya kila siku kwa mtindo wa burudani.
Mashabiki wengi wameonekana kuhusika kwenye maoni, wakichangia kwa vicheko na wengine kukubaliana naye kuwa siku hizi ma-ex wanaachana “kisomi” sana bila hata drama za kusimulia.
Kwa kifupi, Kiredio ameendelea kuthibitisha kuwa yeye ni miongoni mwa wabunifu wanaojua kugeuza maisha ya kawaida kuwa content ya kuchekesha hasa msimu huu wa Valentine.

Post a Comment