MSANII wa
filamu za Kibongo na aliyewahi kujizolea umaarufu mkubwa kama muuza sura
kwenye video mbalimbali za muziki, Asha Salum maarufu kama ‘Kidoa’, @kidoasalum ameibua gumzo jipya mitandaoni baada ya kuanza kuonyesha mabadiliko makubwa ya maisha yake kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Kwa
siku za hivi karibuni, Kidoa amekuwa akichapisha picha na video
zinazoonyesha maisha ya kujiachia na starehe, huku baadhi ya maudhui
hayo yakitajwa na mashabiki kuwa ya “tata” na yanayoibua mjadala mkubwa.
Muonekano
wake mpya pamoja na aina ya post anazoweka zimeanza kuwashangaza wengi,
hasa wale waliomzoea kama msanii mtulivu na mwenye taswira tofauti na
anayoionyesha sasa.
Mbali na picha hizo, Kidoa pia ameonekana
akifurahia maisha ya mapumziko katika maeneo mbalimbali ya kitalii,
ikiwemo Zanzibar, ambako amekuwa akishiriki matukio, matembezi ya
fukweni na kujionyesha akiwa katika hali ya furaha bila kujali maneno ya
wakosoaji.
Hatua hiyo imeonekana kama ishara ya kujiamini na kuamua kuishi maisha yake kwa masharti yake mwenyewe.
Wakati
mijadala ikiendelea kushika kasi, Kidoa aliongeza mafuta kwenye moto
baada ya kuandika ujumbe wenye utata kupitia Instagram, akisema:
“Kama dhambi zako hazikupe pesa basi hayo ni matumizi mabaya ya dhambi.”
Kauli hiyo ilisambaa kwa kasi na kuzua tafsiri tofauti miongoni mwa watumiaji wa mitandao.
Post a Comment