ad

ad

EPL Yapamba Moto Leo: Villa, City na Liverpool Watafuta Pointi Muhimu

 


 Ligi Kuu England (EPL) inaendelea leo kwa michezo kadhaa ya kusisimua huku timu mbalimbali zikisaka pointi muhimu katika mbio za kupanda nafasi kwenye msimamo wa ligi.

Katika moja ya michezo inayosubiriwa kwa hamu, Aston Villa watashuka dimbani kumenyana na Brighton, pambano linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa licha ya tofauti ya pointi 15 zilizopo kati ya timu hizo. Villa watajaribu kutumia uwanja wao wa nyumbani kujihakikishia matokeo mazuri, huku Brighton wakisaka kushtua wenyeji.

Macho pia yataelekezwa katika dimba la Etihad, ambapo mabingwa watetezi Manchester City wataikaribisha Fulham. Katika mechi ya kwanza ya msimu huu, vijana wa Pep Guardiola waliibuka na ushindi, lakini Fulham wataingia wakiwa na dhamira ya kulipa kisasi na kuharibu rekodi ya City nyumbani.

Wakati huohuo, Liverpool watakuwa ugenini kumenyana na Sunderland katika mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu. Sunderland wapo nafasi ya nane, huku Liverpool wakiwa nafasi ya sita, tofauti ikiwa ni pointi tatu pekee. Hii inaifanya mechi hiyo kuwa muhimu kwa Liverpool ambao wanahitaji ushindi ili kujiweka karibu zaidi na nafasi za kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kwa ujumla, siku ya leo mashabiki wa soka wanatarajiwa kushuhudia dakika 90 za presha, mabao na burudani tele katika viwanja mbalimbali vya England.

No comments

Powered by Blogger.