Wastara amwaga chozi akiaga kwenda kutibiwa ‘Sijawahi kuchangiwa na Watanzania’ (Video)
Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Wastara ameondoka nchini kuelekea India kwa ajili ya matibabu ya mguu wake ulioanza kumsumbua mwishoni mwa mwaka jana huku akiwashukuru watanazania na Vyombo vya Habari kwa kuwa pamoja naye kipindi alivyokuwa akihitaji msaada wa fedha.
Na alipoulizwa kuhusu tuhuma za kutumia fedha za matibabu kwa starehe kama alivyowahi kuchangiwa kipindi cha nyuma na kwenda Dubai, Wastara amesema hajawahi kuchangiwa na Watanzania bali alisaidiwa Makamu wa Rais na hakutumia kwa matumizi mengine.
“Kwanza niseme sijawahi kuchangiwa na Watanzania mimi kama mimi, mara ya kwanza nilipoumwa aliyenichangia asilimia kubwa alikuwa ni Makamu wa Rais, na uzuri ni kwamba mpaka nafika hospitalini nilikuwa nampigia simu. Kilichosababisha watu waseme baada ya kufika hospitali kama hivi ninavyokwambia wiki tatu linapotokea tatizo kama umefanyiwa Oparesheni au upasuaji wowote niliambiwa unauwezo wa kukaa au kuishi kwenye hoteli karibu na hospitali..Ndipo watu wa karibu yangu wa Oman wakawa wamenipa Visa nikaenda kukaa huko kwa muda.“ameongea Wastara.
Post a Comment