Sugu na Masonga waachiwa kwa dhamana....Hukumu Yao ni February 26
Mahakama
ya Hakimu Mkazi-Mbeya imewaachia kwa dhamana washtakiwa Mbunge wa Mbeya
Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini, Emmanuel Masonga katika kesi inayowakabili ya kutumia lugha ya
fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.
Sugu
na Masonga wamekaa mahabusu kwa muda wa siku 24 baada ya kunyimwa
dhamana na mahakama hiyo kutokana na hoja za upande wa Jamhuri.
Hakimu
Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite amewaachia kwa dhamana wawili
baada ya Wakili upande wa utetezi, Peter Kibatala kuiambia mahakama hiyo
kwamba imeshafunga ushahidi wake ambapo mashahidi sita walitoa ushahidi
wao.
Mawakili wa pande zote mbili walikubaliana kwamba Februari 19 watawasilisha majumuisho ya shauri hilo mahakamani hapo.
Hakimu Mteite amekubaliana na hoja hiyo ya mawakili na kusema hukumu ya kesi hiyo itatolewa Februari26 mwaka huu.
"Washtakiwa
wote wanaachiwa kwa dhamana, na kila mmoja atajidhamini mwenyewe kwa
hati ya dhamana ya maneno ya Sh5 milioni kwa kila mmoja.
Post a Comment