ad

ad

Bocco: Mimi, Okwi Hatupoi Wapinzani Watakoma

Mshambuliaji na nahodha wa Simba, John Bocco (aliyejifunga kitambaa mkononi) akiwa na Mganda, Emmanuel Okwi (kushoto).

MSHAMBULIAJI na nahodha wa Simba, John Bocco ameshindwa kuzuia hisia zake na kutamka kuwa kama akiendelea kupangwa na Mganda, Emmanuel Okwi kwenye mechi, basi wapinzani watakoma.

Hayo, aliyasema mara baada ya mechi ya Ligi Kuu Bara kumalizika dhidi ya Azam FC kwa timu yao kupata ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Okwi akiunganisha krosi safi ya Mghana, Asante Kwasi.

Bao hilo liliisaidia timu hiyo kuendelea kukaa kileleni ikiongoza kwa idadi ya pointi 41 juu ya Yanga wenye pointi
34 na Azam 33.


Akizungumza Bocco alisema anapenda kucheza na mchezaji wa aina ya Okwi ndani ya uwanja kutokana na aina yake ya uchezaji huku akitimiza majukumu yake ya kufunga na kutengeneza mabao. 

Bocco alisema anajivunia kucheza na mshambuliaji wa aina hiyo huku akiwa na matarajio makubwa ya kuendelea kuifungia Simba katika mechi zijazo za ligi kuu na michuano ya kimataifa.

“Najivunia sana kucheza na mchezaji wa aina hii ya Okwi, niseme ni kati ya wachezaji wenye viwango vizuri ambao mimi ninatamani kuendelea kucheza nao pamoja.

“Uwepo wake uwanjani unanifanya nicheze kwa kujituma nikiamini nitapata matokeo mazuri kama ilivyokuwa tulivyocheza na Azam katika mechi hii iliyopita.

 “Mechi ilikuwa ngumu kama mlivyoona, lakini alifunga bao kwa wakati sahihi katika mechi muhimu ambayo Simba ilizihitaji pointi hizo muhimu katika kuelekea kuuchukua ubingwa huu wa ligi,” alisema Bocco.

Aidha, mshambuliaji huyo hakuishia hapo, aliendelea kummwagia sifa mshambuliaji huyo kwa kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram kuweka picha yake na kutamka: “Huwa namuitaga Emma, respect broo, binafsi najivunia kucheza na mchezaji wa kiwango chako, asante bro kwa kutupatia pointi tatu muhimu kwenye mechi muhimu kwa wakati sahihi.

No comments

Powered by Blogger.