Nape Nnauye aipa changamoto Serikali
Mbunge
Nape Nnauye leo Bungeni ameipa changamoto Serikali juu ya gharama za
kuunganisha umeme na kuishauri kuendelea kuchaji elfu 27,000 hata baada
ya mradi wa REA kupita ambapo wataanza kuchaji 177,000 kuunganisha
umeme.
Nape Nnauye ametoa ushauri huo alipopata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza Bungeni kwenda kwenye Wizara ya Nishati
"Kwanza
niipongeze Serikali chini ya Wizara ya Nishati kwa kazi nzuri
wanayofanya ya usambazaji mzuri wa umeme vijijini hasa REA awamu ya 3,
kwa kuwa gharama za kuunganisha umeme wakati mradi unaendelea ni elfu
27,000 na mradi ukipita ni 177,000 na kwa kuwa idadi kubwa na nzuri ya
watumiaji wa umeme ni biashara nzuri kwa TANESCO kwanini bei hii isiwe
moja ya elfu 27" alisema Nape Nnauye
Hata
hivyo Nape Nnauye aliendelea kusisitiza kuwa kama jambo hilo
halitawezekana basi REA waendelee na uwekaji wa nguzo na miundombinu na
TANESCO wafanye kazi moja ya kupeleka umeme na kukusanya kodi baada ya
kupeleka umeme.
Naibu
Waziri Wizara ya Nishati alijibu hoja hiyo na kudai kuwa amepokea
ushauri huo wa Mbunge wa Mtama na kuwa atapeleka katika ngazi zingine na
kuona Serikali nini itafanya
"Wazo
alilosema Kaka yangu Nape Nnauye linapokelewa na litafanyiwa kazi kwani
ni la msingi kwa sababu Wizara yetu na shirika letu la TANESCO na wadau
wengine wa nishati tunauza bidhaa hii hivyo ni vema tunapouza tupate
wateja wengi ili tupate mapato na kuendesha shughuli mbalimbali na
uwekezaji mpya wa maeneoya nishati"
===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )