Msigwa amchana Kigwangala Bungeni
Mbunge
wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mhe. Peter Msigwa amefunguka na
kumchana Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala na kudai
kuwa anafanya kazi kwa mizuka na mihemko na kuisumbua sekta ya Utalii na
Maliasili nchini.
Msigwa
amesema hayo wakatii alipokuwa akichangia bungeni taarifa ya Kamati ya
Ardhi, Maliasili na Utalii na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji, mjini
Dodoma na kudai kuwa Mawaziri vijana wamekuwa na mihemko.
"Niwashauri
hawa Mawaziri vijana fursa 'opportunity is atrracted by talent, skills,
perfomance and abillity. Show your talent and abillity,m people will
love you'
"Hawa
Mawaziri wa zamani hawa kwa mfano Lukuvi, Tizeba tunawaona wakijibu
hoja wanajibu hoja siyo za kimihemko kiasi kwamba unaridhika hata Waziri
akikujibu unapenda lakini Mawaziri vijana wengi mnaonekana mnayofanya
katika Serikali hii kiasi kwamba Serikali ijayo muonekane hamna tija"
kwa sababu mna mihemko sana"
Mbali
na hilo Msigwa alikwenda mbali zaidi na kumnyooshea mkono Waziri wa
Maliasili na Utalii na kudai amekuwa na maamuzi ya ajabu jambo ambalo
linapelekea kiongozi huyo kuivuruga Wizara hiyo.
"Utalii
huu umejengwa kwa muda mrefu sana na akitokea mtu mmoja anaamua kufanya
tu kwa kutafuta umaarufu atauvuruga kwa muda mfupi sana
"
Utalii kwenye pato la taifa unaingiza asilimia 20 na forex ni kubwa
inatokana na utalii kwa hiyo hicho si kitu kimoja mtu anaweza kuamka leo
anasema nimeharibu na hii diplomasia ya kiuchumi inategemea sana na
kutabirika, wawezekaji huko nje wanataka kuona kunatabirika wao kufanya
biashara zao.
"Haiwezekani
huyu Waziri anatoa amri mpaka mapolisi wanamkataa anashindwa hata
kuwasiliana na Waziri wake wa Mambo ya Ndani, huyu huyu Waziri anatoa
amri anapingana na Waziri wa Ardhi, huyu huyu Waziri mmoja anapingana na
Waziri wa Uvuvi hatuwezi kuwa na Mawaziri ambao wanakuwa na mizuka na
kufanya kazi kwa mizuka wote kama tunalipenda taifa letu tufanye kazi
kwa kupendana" alisisitiza Mchungaji Msigwa
Post a Comment