CCM yazungumzia kutekwa diwani wa CHADEMA
Mbunge
wa Muleba Kusini (CCM), Prof. Anna Tibaijuka amefunguka na kusema kuwa
CCM hakihusiki kivyovyote vile na kutekwa kwa mgombea wa Udiwani wa
CHADEMA Kata ya Buhaganza , Nelson Athanas ambaye alipatikana Februari
5, 2018 akiwa hajitambui.
Tibaijuka
amedai kuwa kuwekuwepo na tetesi kuwa chama chake kimehusika na kitendo
hicho cha kinyama na kudai kuwa hilo ni lengo la kutaka kuvuruga
uchaguzi huo hivyo amesisitiza kuwa chama chake hakihusiki na unyama
huo.
"Kamati
ya siasa ya wilaya ya Muleba imeamua kuwajulisha wananchi rasmi na
wapiga kura wa Kata ya Buhaganza na Umma wa Watanzania kiumjula kwamba
Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakiusiki kwa lolote lile na tuhuma hizo
zinazoongozwa kwake na viongozi wake kwa nia mbaya ya kuwachafua na
kukichafua chama na kuvuruga uchaguzi baada ya kuzidiwa.
"CCM
kimejitayarisha vyema kwa ushindani na kinaamini mgombea wake Bi.
Jenitha Tibihenda anatosha hivyo hakuna haja ya kumteka mshindani wake
yoyote yule tupo imara" alisema Tibaijuka
Aidha
Tibaijuka alivitaka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa tukio hilo
kwa haraka ili watu waliotenda tukio hilo ovu waweze kupatikana kwa
haraka na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mgombea
wa udiwani Kata ya Buhangaza, Muleba (CHADEMA), Athanasio Makoti
aliyekuwa amepotea tangu Februari 2, 2018 alipatikana Februari 5, 2018
akiwa hajitambui, CHADEMA imesema alitupwa barabarani maeneo ya
Hospitali ya Kagondo na sasa aendelea kupatiwa matibabu.
Post a Comment