ad

ad

Breaking News: Tambwe Hizza wa Chadema Afariki Dunia

Kada wa Chadema, Tambwe Hizza, enzi za uhai wake

 KADA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tambwe Hizza, amefariki dunia leo asubuhi nyumbani kwake akiwa amelala, msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene, amethibitisha na kuongeza kwamba mwili wake umepelekwa Hospitali ya Temeke Dar es Salaam asubuhi hii. Kwa mujibu wa Chadema, marehemu Hiza alikuwa kwenye moja ya vikao vya chama hicho hadi jana saa tano usiku wa kuamkia leo.   [caption id="attachment_196938" align="alignnone" width="1200"] ...Akiwa katika moja ya mikutano ya Chadema

  Marehemu Tambwe Hizza amefariki akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu na alikuwa pia mmoja wa waratibu wa kampeni za chama hicho katika jimbo la Kinindoni Hizza anafahamika sana kwa siasa zake akiwa CUF, baadae alihamia CCM na kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa CCM na 2015 aliamua kuondoka CCM na kuhamia CHADEMA.

No comments

Powered by Blogger.