ad

ad

Simba Yamkaribisha Kocha Mpya kwa Ushindi, Yaipiga 4-0 Singida Taifa

Wakati Singida United ikitarajiwa kutoa upinzani mkali dhidi ya Simba, imejikuta ikichezea kichapo cha bao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara. Simba ikiwa imetoka kufanya vibaya kwenye mashindano ya Mapinduzi kwa kutolewa hatua ya makundi, wameishangaza Singida ambayo ilifanya kweli Mapinduzi Cup na kufika hatua ya nusu fainali huku ikiwa imepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Azam. Singida United ilizivimbia Azam na Yanga kwenye michezo ya ligi na kuzilazimisha timu hizo kutoka sare. Walilazimishwa sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Azam kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma kabla ya kuibana Yanga na kutoka suluhu uwanja wa Namfua, Singida. Singida United 1-1 Azam Singida United 0-0 Yanga Simba 4-0 Singida United Emanuel Okwi ambaye hakuonekana kwenye mechi kadhaa za ligi pamoja na mashindano ya Mapinduzi Cup amerejea vizuri, baada ya kufunga magoli mawili dhidi ya Singida Unite akitokea benchi dakika ya 66 kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mzamiru Yassin.

No comments

Powered by Blogger.