ILE ISHU YA SIMBA KUANDIKA BARUA WAKITAKA MECHI YAO NA AZAM ISOGEZWE IKO HIVI...
Simba
yenye pointi 35, inachuana vikali na Azam wenye 30 katika msimamo wa
ligi na Mabingwa watetezi Yanga waliovuna 28, katika kuliwania taji hilo
la ubingwa la ligi.
Mkuu
wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Haji Manara alisema
ratiba yao inawapa ugumu kutokana na akili na nguvu zao kuzielekeza
kwenye michuano ya kimataifa na Simba imepangwa kucheza Gendarmerie
Nationale ya Djibouti kati ya Februari 9-11, mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Manara
alisema, ratiba hiyo inawapa ugumu kwani Simba itacheza na Ruvu
Shooting Februari 4 na kucheza na Azam kabla ya kwenda Shinyanga kucheza
na Mwadui huku wakiusubiria mchezo wao wa kimataifa.
“Mipango
ya Simba ni kufika mbali katika michuano ya Afrika na hiyo ndiyo sababu
ya sisi kumchukua kocha Mfaransa, Lechantre (Pierre) ambaye amewahi
kuipa ubingwa wa Afcon, Cameroon mwaka 2000.
“Hivyo,
basi kama uongozi tumeiomba Bodi ya Ligi kusogeza mbele mchezo wetu
dhidi ya Azam ili kutupa nafasi ya kujiandaa na mechi yetu ya kimataifa
dhidi ya Wadjibout kwa kuwa tunaona ratiba inabana sana.
“Tupo
katika hatua ya mwisho kwa ajili ya kuiandikia bodi ya ligi ili
kuwafahamisha mchezo huo usogezwe mbele na kikubwa tunataka kuona Simba
ikifanya vema katia michuano hii ya mikubwa Afrika, tunaamini busura
itatumika,”alisema Manara.
Post a Comment