ad

ad

Yanga Kuanza Na Timu Kutoka Shelisheli Ligi Ya Mabingwa Afrika

Droo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa hatua ya awali imepangwa mchana wa leo ambapo Yanga ni moja ya timu iliyohusika katika droo hiyo.

Yanga imepangwa kucheza dhidi ya St Louis Suns United ya Shelisheli katika hatua ya awali, mchezo wa kwanza itakuwa Februari 9-11, 2017.

Mchezo wa pili unatarajiwa kupigwa kati ya Februari 16 hadi 18.
Mechi ya kwanza ya michuano hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam, mechi ya pili Yanga itakuwa ugenini.

Baada ya ya michezo hiyo miwili, Yanga ikifanikiwa kusonga mbele itakutana na mshindi wa mechi kati ya Township Roller (Botswana) dhidi ya El Merreikh (Sudan).

Katika hatua hiyo, timu tano kubwa hazitahusika kushiriki kwenye droo ya awali (Preliminary Round) kutokana na mafanikio yao katika michuano hiyo ni:
1. TP Mazembe,
2. Wydad Casablanca,
3. Al Ahly,
4. ES Sahel na 
5. Mamelodi Sundowns

No comments

Powered by Blogger.