ad

ad

Wadada Wanaodaiwa Kujihusisha na Usagaji Waachiwa Kortini

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mwanza imewaachia kwa dhamana wadada wawili waliokamatwa kwa tuhuma zinazoashiria kujihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja baada ya picha zao kusambaa wakivalishana ‘pete ya uchumba’.
Wadada hao, na wenzao wawili wameachiwa kwa dhamana ya Tsh. milioni 6 kila mmoja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kutupilia mbali hoja za kuzuia dhamana zao zilizowasilishwa na upande wa Jamhuri.

Shauri la dhama hiyo limeamriwa leo Desemba 15 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Wilbert Chuma baada ya kukubaliana na hoja za mawakili wa utetezi, Mashaka Tuguta, Ogastini Kulwa na Jebra Kambole kuwa hoja zilizowasilishwa na upande wa mashtaka ni dhaifu.

Katika kesi hiyo, washtakiwa ni Milembe Suleiman na Janeth Shonza ambaye ni mwanafunzi wa kozi ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) wanaodaiwa kuvishana pete ya uchumba licha ya wote wawili kuwa na jinsia ya kike. Wengine wanaokabiriwa katika kesi hiyo ni Aneth Mkuki anayedaiwa kufanikisha sherehe wanawake hao kuvishana pete na Richard Fabian, anayekabiriwa na kwa kosa la kusambaza video za tukio hilo mitandaoni.

Hakimu Wilbert Chuma amesema Mahakama haiwezi kufanyia kazi maelezo na vitu vya mashaka na uvumi kuwa washtakiwa wanaweza kudhuriwa na jamii iliyochukizwa na kitendo wanachoshtakiwa nacho.

“Huu ni uamuzi wa Mahakama kuwa dhamana ni haki ya kisheria ya washtakiwa, upande wa mashtaka umeshindwa kuwasilisha hoja za msingi kwa nini wanyimwe dhamana zaidi ya kutoa hoja za hisia kuwa wakiachiwa watadhuriwa na jamii bila kueleza watadhurikaje na nani haswa atawadhuru?” alisema Hakimu Chuma

.
Aidha washtakiwa hao wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja mwenye kitambulisho na barua ya utambulisho kutoka mamlaka inayotambulika kisheria pamoja na kusaini hati ya dhamana ya Sh Milioni 6 huku shauri likiahirishwa hadi Januari 8, 2018.

No comments

Powered by Blogger.