Nandy Amshukuru Naibu Spika kwa Kuusifia Wimbo wake wa Kivuruge
Msanii
wa muziki wa bongo fleva Nandy, amesema anamshukuru Naibu Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa pongezi alizompa, kwani ni
kitu ambacho hakikutarajia.
Nandy amesema kuwa ni kitu cha faraja kuona anapongezwa na kiongozi mkubwa serikalini, hivyo kimempa faraja.
“Nimefurahi
kwa sababu ni mtu ambaye ananisapoti sana, na imenipa faraja sana kwani
sikutarajia, kwa sababu mi nilitumiwa kwenye group nikaiona, basi
nikampigia simu nikaongea naye nikamshukuru”, amesema Nandy.
Jana
Naibu Spika Tulia Ackson alipost kwenye instagram yake akimpongeza
Nandy kwa jitihada zake anazozifanya kwenye kazi yake ya sana ya muziki.
Post a Comment