Nandy Amshukuru Naibu Spika kwa Kuusifia Wimbo wake wa Kivuruge
Shirikisho
la Soka nchini (TFF), limeingia mkataba mnono na Kampuni ya Macron
ambayo kuanzia sasa ndiyo mdhamini mkuu wa jezi za timu zote za Taifa;
Taifa Stars, Twiga Stars na Serengeti Boys.
Aidha,
udhamini huo wa miaka miwili wenye thamani ya Euro 700,000 zaidi ya Sh.
bilioni 1.8 za Tanzania umegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni
jezi na vifaa vingine vya michezo, pamoja na fedha taslimu.
Akizungumza
wakati wa utiaji rasmi saini ya makubaliano hayo wakati wa mkutano wa
TFF na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, Kaimu Katibu Mkuu wa
shirikisho hilo, Wilfred Kidau, alisema hiii ni mara ya kwanza kwa timu
za Taifa kupata mkataba mnono kama huo.
"Kwa
mwaka tutakuwa tukipata euro 150,000 ambapo kwa miaka miwili ni euro
300,000 (takriban Sh. milioni 800) hizo zikiwa ni mbali ya kupewa jezi
na vifaa vingine, hii ni mara ya kwanza kwa timu zetu za taifa kupata
udhamini wa jezi mkubwa kama huu," alisema Kidau.
Kwa
upande wa Rais wa TFF, alisema bado wanaendelea kutafuta wadhamini kwa
timu hiyo na ile ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ambayo haihusiki
katika udhamini huo wa Macron.
"Mchakato
huu umechukua muda mrefu na walikuwapo washindani wengi, lakini Kampuni
ya Macron ndiyo imeshinda, na hatuishii hapo tu bado tunahitaji
wadhamini wengine watakaoidhamini pia Kilimanjaro Stars.
"Kuna
mengi tutakayofaidika katika mkataba huu, kwani pia tutakuwa tukipata
sehemu ya mauzo ya jezi za timu ya Taifa na pia sasa itakuwa ni vigumu
kutengenezwa na kuuzwa kiholela," alisema Karia.
Aliongeza
kwa kufafanua kuwa awali ilikuwa vigumu kudhibiti watengenezaji na
wauzaji holela kwa kuwa hata nembo ya TFF ilikuwa haijasajiliwa jambo
ambalo kwa sasa limefanyika kabla ya kukamilisha mchakato huo wa
udhamini.
Karia
alisema faida ya uuzwaji wa jezi hiyo itaonekana kwa sasa kwa kuwa
anaamini kutokana na Rais John Magufuli, kudhibiti uingizwaji uholela wa
bidhaa nchini kwa kuimarisha ulinzi mipakani na bandarini, itakuwa ni
vigumu kwa wale waliokuwa wakitumia ujanja huo kujinufaisha.
Post a Comment