ad

ad

Michirizi Ya Damu - 02


“Hahah! Mimi mzee wa madili! Ni jambo la kumshukuru sana Mungu,” alisema Godfrey, Theresa akasimama na kumkumbatia.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake kila siku, alikuwa mtu wa biashara, alihangaika huku na kule kutafuta pesa, hakutaka kukaa nyumbani, alikuwa akipambana huku na kule kutafuta pesa kwani aliamini kwamba hasingeweza kufanikiwa kama angekaa tu nyumbani hivyo kupambana kwa kila hali kutafuta pesa.
Hakuchoka, hakulala, kila siku alikuwa akitoka huku na kule. Hakutaka kuona akishindwa, alipambana kila siku na kumfanya kuwa miongoni mwa mabilionea wakubwa nchini Tanzania.
Walizungumza mambo mengi, wakati akiwa kwenye mazungumzo hayo, ghafla akasikia simu yake ikianza kuita, alipoangalia jina, ilikuwa simu kutoka kwa mfanyabiashara mwenzake, Majeed Khan, Muhindi aliyekuwa akipanga naye mipango mikubwa ya kibiashara.
Hakukuwa na usikivu mahali hapo, akamuonyeshea mkewe kioo cha simu na kumwambia kwamba alitakiwa kutoka hapo na kwenda kuzungumza naye kitu ambacho hakikuwa na tatizo lolote lile.
Akatoka sehemu hiyo iliyokuwa ikisikika muziki kwa sauti ya juu na kwenda upande mwingine kabisa na kuanza kuzungumza naye. Walizungumza kwa dakika kadhaa huku wakicheka kwani Khan ndiye aliyekuwa akifanya naye michongo yote ya biashara.
“Samahani kaka!” alisema mwanaume mmoja kwa sauti nyembamba huku akitaka kupita mbele ya Godfrey kwani pale alipokuwa amesimama, aliziba njia kutoka na umbo lake kuwa kubwa na sehemu hiyo kuwa ndogo.
“Hakuna shida!”
Akarudi kwa nyuma kidogo na kumpisha mwanaume huyo ambaye naye alipita upandeupande huku akimpa mgongo Godfrey, kilichomshangaza, bila aibu yoyote ile mwanaume huyo akamgusa eneo la zipu na kumtekenya kidogo.
“Wewe vipi?” aliuliza Godfrey lakini mwanaume huyo hakuzungumza kitu zaidi ya kutoa tabasamu na kuelekea alipokuwa akielekea.
Godfrey alibaki pale alipokuwa, alisimama huku akimwangalia mwanaume yule. Kwa kumwangalia, alionekana kama mtu aliyekamilika lakini alipomwangalia vizuri, akagundua kwamba hakuwa sawa, alikuwa mwanaume aliyekuwa na tabia za kikekike.
Kichwa chake kilichanganyikiwa. Katika maisha yake yote, Godfrey hakuwa mtu wa wanawake, hata kumuoa Theresa ni kwa sababu tu alitakiwa kufanya hivyo.
Katika utajiri mkubwa aliokuwa nao, hakuwa akitembea na wanawake, wengi walijigonga kwake na kumwambia kuhusu hisia zao lakini hakuwa akishughulika nao hata kidogo.
Ugonjwa wake mkubwa ulikuwa ni wa kutembea na wanaume wenzake, alipenda mambo ya mapenzi ya jinsia moja, kila alipokuwa akimuona mwanaume aliyekuwa kwenye hali ya uanawake, alichanganyikiwa na wakati mwingine alikuwa tayari kufanya kitu chochote kile kumpata.
“Haiwezekani! Huyu simuachi,” alijisemea huku akimwangalia mwanaume yule aliyevalia kipensi kifupi, nywele zake alizipaka kalikiti na macho yake alikuwa akiyarembua mithili ya mwanamke aliyekula kungu.
“Call me my sweetie,” (nipigie mpenzi) alisema mwanaume yule kwa sauti nyembemba zaidi huku akiweka kidole cha gumba karibu na sikio na kidogo karibu na mdomo wake kumaanisha kwamba alitaka kupigiwa simu.
“I ain’t got your number,” (sina namba yako!) alisema Godfrey huku akimwangalia mwanaume huyo aliyeingia ndani ya gari.
“I will call you,” (nitakupigia) alisema mwanaume huyo, akawasha gari na kuondoka mahali hapo.
Godfrey akarudi kwenye kiti chake huku akionekana kuchanganyikiwa mno, kichwa chake kilikuwa kikimuwaza mwanaume tata aliyekutana naye.
Alikuwa kwenye mawazo tele, huo ndiyo ulikuwa ugonjwa wake, hakuwa na hamu na wanawake hata mara moja. Kitendo cha kukutana na mwanaume huyo mwenye sura nzuri kilimpagawisha kupita kawaida.
Theresa alimwangalia mume wake, aligundua kwamba kulikuwa na tatizo, hakuwa sawa, alionekana kuwa kwenye lindi la mawazo kupita kawaida. Hakutaka kumuacha hivyo, alimuuliza tatizo lilikuwa nini lakini hakujibu zaidi ya kumwambia kwamba alikuwa kawaida.
“Haiwezekani! Niambie kuna nini mpenzi,” alimwambia mumewe.
“Hakuna kitu!”
“Kweli?”
“Ndiyo!”
“Dili bado lipo mezani au wamelifuta?”
“Yote yapo mezani mke wangu!”
Hawakukaa mahali hapo, wakaondoka. Muda wote alikuwa akiangalia simu yake, alitaka kuona mwanaume huyo akimpigia na kumwambia mahali alipokuwa akipatikana kwani alijua kabisa kwamba asingelala, asingekula kwa sababu yake.
Kama ambavyo mwanaume anayependa wanawake anapokutana na msichana mzuri, akampa namba na kutaka kupigiwa, jinsi alivyokuwa akisubiri kwa presha ndivyo ambavyo alivyokuwa akisubiri kwa presha kubwa.
“Mbona hanipigii zaidi ya kunitamanisha tu! Mtoto ameumbika sana, ana miguu membamba lakini hapa kiunoni amekaa poa sana. Naomba anipigie tu! Ila namba yangu anayo kweli au aliniambia vile kama kunitega?” alijiuliza Godfrey, hakupata jibu.
Aliendelea kusubiri, aliisubiria simu ya mwanaume huyo zaidi ya alivyokuwa akisubiri dili za kuanza kufanya biashara zake. Siku ya kwanza ikakatika, ya pili, ya tatu mpaka wiki hakuwa amepigiwa simu kitu kilichomfanya kuukosa amani, hata safari zake za kwenda Marekani na Uarabuni hazikuwa na furaha tena, muda wote moyo wake ulikuwa ukimuwaza mwanaume huyo tu aliyekuwa na muonekano kama wa kike, alikuwa shoga.
****
Godfrey aliendelea kusubiri mpaka akakata tamaa. Miezi mitatu ilipita lakini hakuwa amepigiwa simu na mwanaume huyo hivyo kuona kwamba ilishindikana hivyo kuendelea na maisha yake.
Maisha yake hayakubadilika, kila siku aliwatamani wanaume wenzake, hakuwa na muda na wanawake, kwake, maisha yalionekana kuwa tofauti, wakati wanaume wenzake wakiwatamani wanawake, kwake, aliwatamani sana wanaume kuliko wanawake.
Alikwenda nchini Marekani, huko, kazi yake kubwa ilikuwa ni kulala na wanaume na kufanya nao mapenzi. Alijua kwamba ilikuwa dhambi kubwa lakini hakutaka kuacha, yalikuwa ni maisha ambayo aliyazoea, ikawa tabia yake na kumganda kama ruba.
Baada ya kupita miezi sita tena huku akiwa barani Asia ndipo akatumiwa meseji katika akaunti yake ya WhatsApp, harakaharaka akaifungua na kuisoma, alitumiwa kupitia namba ngeni na ujumbe aliotumiwa ulikuwa mfupi tu uliosomeka ‘Miladiva’.
Kitu cha kwanza kabisa kumjia kichwani mwake kilikuwa ni kukumbuka kitu kilichotokea kwenye ufukwe huo. Alikumbuka kwamba mara ya mwisho kwenda katika ufukwe huo ni miezi kadhaa iliyopita ambapo alikwenda pamoja na familia yake.
Hakujua ujumbe huo ulimaanisha nini lakini alipouliza, akatumiwa ujumbe mwingine mfupi uliosomeka ‘Nipigie’, hapo ndipo akakumbuka, picha ya mwanaume tata yule aliyemwambia ampigie ikamjia kichwani mwake, hakutaka kuchelewa, akamtumia meseji ya kulalamika kwamba ilichukua muda mrefu mpaka kumtafuta.
“Nilikuwa bize sana. Ila nimekumiss baba watoto,” aliusoma ujumbe huo, mwili ukamsisimka.
“Kweli?” aliuliza.
“Ndiyo! Naomba nikuone jamani!” aliusoma ujumbe huo ambao uliambatanishwa na sauti iliyorekodiwa, alipoifungua, ilikuwa sauti ya mwanaume huyo iliyokuwa ikilalamika kimahaba, tena mbali na hiyo, alimwambia kwamba alihitaji mpenzi wa kudumu kwani wapenzi wote aliokuwa nao waliishia kumtenda tu, hawakuwa na mapenzi ya dhati.
“Nipo kwa ajili yako! Nitakulinda mpenzi! Naomba kuonana nawe nikifika Tanzania,” alimwambia.
“Kwani upo wapi?”
“Nipo Kuwait, kuna kitu nimefuata.”
“Basi sawa baba watoto! Nakupenda!”
“Nakupenda pia. Mwaaaaah!”
“Mwaaaah!”
Wakaagana, Godfrey hakuamini kama aliwasiliana na mwanaume tata huyo, alibaki hotelini huku akiwa amechanganyikiwa kwa furaha, aliinuka na kuanza kurukaruka, alikuwa na hamu ya kupata mawasiliano na mwanaume huyo na mwisho wa siku alipigiwa na hivyo kuwa na namba yake.
Wakati akiwa anafurahia akasikia simu yake ikilia na alipoifungua akakutana na picha za kihasarahasara alizotumiwa katika akaunti yake ya WhatsApp ambazo zilimuonyesha mwanaume huyo akiwa katika mikao ya hatarihatari.
Japokuwa alikwenda Kuwait kukaa kwa wiki moja na kutakiwa kwenda nchini Uingereza lakini wiki moja akaiona kuwa kama mwaka, kila siku kazi yake ilikuwa ni kuangalia kalenda, hakukuwa na kipindi alichokiona siku kwenda taratibu kama kipindi hicho.
Baada ya wiki moja kukatika na kutakiwa kuelekea nchini Uingereza, hakutaka kwenda huko, hakukubali, mtu aliyekuwa akimkumbuka alikuwa mwanaume huyo aliyeitwa Fareed Hassan lakini alilibadilisha jina lake na kujiita Anti Farida.
Alipofika Tanzania, hata kabla ya kuelekea nyumbani kwake, akampigia simu Fareed na kumwambia kwamba alikwishafika nchini Tanzania hivyo alitaka kuonana naye.
“Sawa. Niambie nije wapi mpenzi?”
“Njoo hapa Dragon Fire, nitakuwepo chumba namba 20, ukija niambie niwaambie wakuruhusu,” alisema Godfrey.
Akaelekea katika hoteli hiyo, kwa kuwa alikuwa amekwishaweka oda, akaelekea katika chumba hicho na kuanza kumsubiri Fareed kwa hamu kubwa. Kila wakati alikuwa akimcheki kwenye simu kujua alifikia wapi, alitaka kumuona haraka sana kwani hakukuwa na mtu aliyekuwa na kiu ya kumuona kama mwanaume huyo.
“Nakuja jamaniiiiiii!” alisema Fareed.
“Basi wahi kipenzi! Si unajua nina kiu ya kukuona.”
“Wala usijali senyorita.”
Baada ya nusu saa akafika katika hoteli hiyo, akamwambia kwenye simu kwamba alikuwa mapokezi na hivyo kuwataka wamruhusu na kufanya hivyo. Kila mtu aliyekuwa akimwangalia Fareed, alimshangaa, alionekana kuwa na muonekano wa kike, na hata kama ungeambiwa kwamba mtu huyo alikuwa mwanaume ungebisha.
Alitembea kwa mikogo, alipokuwa akipandisha ngazi, alipandisha kwa mbwembwe huku akijitahidi kujitingisha kwa nyuma. Hakuacha kioo chake, wakati akipandisha ngazi, alikitoa kutoka kwenye mkoba wake, akatoa na lipstiki na kisha kuanza kujipaka, kila mtu aliyemuona, aliuona mwisho wa dunia.
“Jamani dunia imekwisha…” alisikika mteja mmoja.
“Kweli kabisa. Ukiwa na mtoto wa hivi! Wewe muue tu kama alivyofanya baba yake Gey yule mwanamuziki wa Marekani!” alisema jamaa mwingine.
“Kweli kabisa. Mwanaume kama mwanamke!”
“Sasa mbona anaelekea kule, kuna mtu anamsubiri?”
“Ndiyo! Kuna mshua ana apointimenti naye,” alisema dada wa mapokezi maneno yaliyomfanya kila mtu kushangaa na wengine kusikitika.
Alipofika katika chumba hicho, hakugonga, akaingia moja kwa moja. Godfrey alipomuona akiingia, akasimama, akamfuata na kisha kumkumbatia kwa furaha, hakuamini kama mwisho wa siku alionana na Fareed ambaye kila siku alikuwa akimwambia jinsi alivyokuwa akimmiss mpaka safari yake ya wiki moja kuonekana kama mwaka mzima.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya Fareed, alikuwa mwanaume tata aliyeanzia tabia hiyo tangu akiwa mdogo. Alikuwa na muonekano mzuri, alikubalika, alijiona kuwa kama msichana mara baada ya kwenda kuishi kwa baba yake mdogo ambaye aliamua kumfanyia kitendo cha ajabu baada ya mkewe kusafiri kwenda Arusha.
Aliuanzia mchezo huyo kwa baba yake mdogo, alisikia maumivu sana kipindi cha kwanza lakini kikafika kipindi ambacho alizoea kabisa, akaharibika, kila kitu kilichokuwa kimetokea kilikuwa siri kubwa.
Hakumwambia mtu lakini alipomchoka baba yake mdogo akaondoka nyumbani na kwenda kufanya matendo hayo nje ya nyumba hiyo. Huko ndipo akakutana na wenzake na kumwambia kwamba tabia hizo zilikuwa zinaingiza fedha kama tu angemtafuta wakala wa kumtafutia Wazungu.
Akakubaliana nao na kumpata wakala ambaye kazi yake ilikuwa ni kumtafutia wanaume sehemu mbalimbali duniani. Alipata mabwana wengi kutoka Ulaya na Marekani. Huko kote alipokuwa akisafiri, alitumiwa tiketi na gharama zote ambapo wakala wake alichukua robo.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake, alipata kiasi kikubwa cha fedha na kwenye maisha yake alikuwa akimiliki nyumba mbili za kifahari, magari, yote hayo yalitokana na biashara yake hiyo.
Alimsikia Godfrey tangu kitambo, aliambiwa mambo mengi kwamba mwanaume huyo alikuwa akihusudu mapenzi ya jinsi moja tena kwa kugawa kiasi kikubwa cha fedha kwa wanaume tata wote aliokuwa akifanya nao mapenzi.
Alichanganyikiwa, alipenda kuwa na pesa, alitaka wanaume wote waliokuwa na pesa wawe upande wake hivyo alichokifanya ni kuanza kumfuatilia.
Akafanikiwa kupata namba yake ya simu, hakutaka kumpigia kwa kuogopa maswali mengi ila alichokifanya ni kuwaambia marafiki zake kwamba popote pale ambapo wangemuona Godfrey basi wampigie simu kumtaarifu.
“Leo nimemuona hapa Miladiva,” alisema rafiki yake kwenye simu.
“Yupo?”
“Ndiyo! Ila na familia yake!”
“Nakuja! Nilivyokuwa na hamu naye. Nakuja!” alisema Fareed na kukata simu.

4
Hakutaka kubaki nyumbani, akaelekea huko na kuonana na mwanaume huyo na kumfanyia kituko cha kumshika katika zipu yake. Godfrey akachanganyikiwa lakini akamwambia kwamba angempigia simu.
Hakutaka kujifanya kuwa na haraka, alijua kwamba mwanaume huyo angekuwa na presha ya kuonana naye, alitaka kuvuta muda mpaka wiki moja iishe ndiyo awasiliane naye.
Wakati akisubiri wiki moja ipite, akaanza kupata madili mengi, akawa mtu wa kuzunguka nchi mbalimbali kufuata wateja kiasi kwamba mpaka miezi yote hiyo inakatika bado alikuwa bize na wateja hao, na aliporudi Tanzania, mtu aliyemjia kichwani mwake alikuwa Godfrey hivyo kumpigia na kuonana naye kisha kufanya kile kilichowafanya wapigiane simu.
“Wewe ni zaidi ya wapenzi wangu wote,” alisema Fareed.
“Kweli?”
“Haki ya Mungu tena. Ninakupenda sana mpenzi! Hakika sijuti kuwa nawe,” alisema Fareed, akachukua mkoba wake, akatoa wanja na kuanza kujipaka vizuri huku akijiangalia kwenye kioo.
“Ninafurahi sana kukutana nawe. Hakika sitokuacha. Nitakuwa radhi kuachana na mke wangu ila si kukuacha wewe,” alisema Godfrey huku akionekana kuchanganyikiwa. Kwa kifupi ni kwamba akatekwa na penzi jipya.
****
Hali ilibadilika, mapenzi ya Godfrey kwa mkewe yakapungua, hakutaka kuwa naye karibu kama ilivyokuwa siku za nyuma, mapenzi yalikuwa kwa mwanaume tata ambaye alikutana naye ufukweni.
Walikuwa wakiwasiliana kama kawaida, mara kwa mara walikutana na hata alipokuwa akienda safari zake za Ulaya, Marekani na nchi nyingine alikuwa akiongozana naye ambapo huko uchafu wao uliendelea.
Fareed aliendelea kufanya mambo yake kama kawaida, alimpenda sana Godfrey, alimpa kila kitu alichotaka lakini siku zote alitamani kutembea na wanaume wengine. Aliijua dunia, alijua nchi zilizokuwa na wanaume tata wengi, watumiaji wa watu hao na hata alipokwenda huko, wakati mwingine alikuwa akimtoroka Godfrey na kujiunga na wenzake kufanya ufuska.
Siku ziliendelea kukatika, walipokuwa wakirudi nchini Tanzania, halikuwa jambo la ajabu kumuona Godfrey akiondoka nyumbani na kurudi baada ya siku tatu. Kila alipokuwa akiulizwa, alikuwa mkali, aligombana na mkewe kisa tu alihisiwa kulala na wanawake wengine.
Mkewe akaanza kupeleleza, aliamini kwamba kwa namna moja au nyingine ilikuwa ni lazima kuwe na mwanamke aliyekuwa akimzuzua mume wake hivyo kumfuatilia.
Alifuatilia kwa kuchukua simu yake nyakati za usiku na kuangalia meseji mbalimbali, hakuweza kugundua, hakuacha, aliendelea kufuatilia watu aliokuwa akiwasiliana nao, wengi walikuwa wanaume lakini kulikuwa na mwanaume mmoja ndiye aliyekuwa akiwasiliana naye sana, huyu aliitwa Fareed.
Mara ya kwanza akahisi kwamba alikuwa msichana aliyembadilisha jina, akaangalia katika mtandao wa simu kwenye huduma ya kifedha kugundua kama hilo lilikuwa jina lake au mumewe alimfanyia mchezo, alipoangalia, akakutana na jina hilohilo, Fareed Hassan.
Hakuwa na hofu na mwanaume huyo, aliendelea kutafuta lakini hakumfuma mumewe kuwa na uhusiano wa siri na mwanamke mwingine. Akauachia moyo wake kumwamini mwanaume huyo, akajiondoa hofu, akaona kwamba kila alipokuwa akiambiwa kwamba alikuwa bize na mambo ya biashara, kweli alikuwa bize.
Siku zikakatika. Kwa Fareed, maisha yalikuwa burudani lakini hakutaka kuendelea kuwa na mwanaume mmoja tu. Alitaka kila mwanaume mwenye mwili mzuri awe wake. Hakuacha kujiremba, alijipamba, alijua kujisafisha na kila alipokuwa, alikuwa akinukia maradhi ya Zenji, alijua kurembua macho, alijua kubinua midomo na zaidi ya yote alijua sana kuzungumza hasa kwa sauti ile ya kike.
Kwa wakati huo, alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda Dubai. Alikuwa akimsindikiza mpenzi wake huyo aliyekuwa akienda kwa mambo ya kibiashara. Alichukua ndege pamoja naye, alivalia mavazi ambayo ilikuwa ni vigumu kugundua kama alikuwa mwanaume, alijiremba, alivalia dela na kichwani alivalia kiremba.
“Unakwenda Dubai?” aliuliza wakala wake aliyeitwa Asteria Kimaro, mwanamke aliyekuwa akiwaunganisha wanawake na wanaume tata kwa wanaume wengi waliokuwa wakiishi Ulaya, Asia na Marekani. Alijenga nyumba nyingi, kununua magari ya kifahari kwa biashara hiyo tu.
“Ndiyo!”
“Kuna wateja wawili wanakuhitaji huko. Nishafanya mawasiliano nao, nakutumia namba zao. Wanakuhitaji sana,” alisema Bi Asteria.
“Haina shida! Ila wana hela?” aliuliza Fareed, yeye alikuwa akifikiria hela tu.
“Eeh! Mtu aishi Dubai, awe mfanyabiashara mkubwa halafu asiwe na pesa! Umeona wapi hiyo! Hao wana hela mpaka wanaumwa!” alisema Bi Asteria.
“Basi sawa. Naomba namba zao!”
Akatumiwa namba hizo. Mwili wake ulikuwa ukiwasha mno, kila alipokaa, akili yake ilikuwa ikifikiria pesa tu. Hakutaka kuona akiishi maisha ya kimasikini, alijitoa maishani mwake, hapokuwa alikuwa akifanya jambo gumu, lenye kujidharirisha lakini hakuwa na jinsi, hayo yalikuwa maisha ambayo aliyachagua na alipaswa kuishi katika maisha hayohayo.
Walipofika Dubai, wakateremka ndani ya ndege, haikuwa mara yake ya kwanza, alikwishawahi kufika mara kadhaa hapo, wakatoka nje na kuchukua gari kisha kuelekea hotelini. Walipofika huko, ilikuwa ni kujiachia tu, walikuwa wakiyafurahia maisha, Godfrey alisahau kama alikuwa na mke, kwake, mwanaume huyo tata alimridhisha mno.
Usiku wa siku hiyo wakati Godfrey akiwa amelala huku amejichokea zake, Fareed akachukua simu yake na kuanza kupiga namba za wanaume aliokuwa amepewa. Alianza na mwanaume wa kwanza, huyu aliitwa Saed Al Muntazir, alikuwa mwanaume mwenye mwili uliojazia, ndevu nyingi, alikuwa mwanaume wa shoka, mweye pesa zake, kama alivyokuwa Godfrey, hata naye tabia yake ilikuwa ileile, kulala na wanaume tata kuliko hata wanawake.
“Nilipewa namba yako!” alisema Fareed, alikuwa amekimbilia chooni kuzungumza na mzee huyo.
“Kutoka wapi?”
“Kwa Asteria…”
“Ooh! Kumbe nini wewe! Hebu nitumie picha zako za utupu zikionyesha ulivyoumbika,” alisema mwanaume huyo.
Hiyo ilikuwa kazi ndogo kwa Fareed, hakutaka kuchelewa, hapohapo akamtumia picha hizo alizokuwa amekaa mikao ya hasarahasara, mwanaume huyo akazipokea, akaanza kuziangalia, mwili wake ukasisimka, hakuamini kama angekutana na mtu mwenye sura nzuri, umbo mashallaah kama alivyokuwa Fareed.
“Njoo hotelini kwangu!”
“Sawa. Nitakuja kesho asubuhi!” alisema Fareed.
“Sawa mpenzi!”
Hakutaka kukaa chooni kwa muda mrefu, akatoka na kurudi chumbani. Alipofika, macho yake yakatua kwa mpenzi wake, Godfrey ambaye alikuwa amekaa kitandani huku akionekana kuwa na hasira kupita kawaida.
Alivimba, alikuwa akipumua kwa hasira, paji lake la uso lilikunja ndita, kwa jinsi alivyoonekana, hakuonekana kuwa kwenye hali ya kawaida. Fareed aligundua kwamba kulikuwa na kitu, akagundua kwamba inawezekana mwanaume huyo aliyasikia mazungumzo yake alivyokuwa chooni, akaogopa kwani kuachwa na mwanaume huyo kulimaanisha angepoteza vitu vingi, starehe zote zingepaa.
Akaanza kumsogelea, hakuzungumza kitu, kwa mbali alionekana kutetemeka lakini hakutaka kulionyesha hilo, hakutaka agundulike kama alikuwa na hofu kubwa. Alipomfikia pale kitandani, akakaa pembeni yake na kuupitisha mkono wake katika bega la Godfrey.
“Tatizo nini mpenzi?” alimuuliza Godfrey.

ITAENDELEA KESHO
https://www.youtube.com/c/KidaniStars

No comments

Powered by Blogger.