ad

ad

Kisa Ujauzito, Odama Apata Kigugumizi!

MWIGIZAJI mwenye kipaji cha aina yake katika tasnia ya filamu nchini, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amepatwa na kigugumizi alipotakiwa kueleza ukweli wa uvumi kwamba ana mimba changa.
Odama alijikuta akipatwa ugonjwa wa ghafla wa kigugumizi baada ya kona ya Star Mix kumbana na kutaka kujua ukweli wa uvumi huo ambapo aliishia kumuomba mwandishi ampe muda wa kufikiria kabla ya kujibu.

“Nipe muda nilitafakari swali lako, lakini kama hutojali tunaweza kuzungumza mambo mengine hilo tukaachana nalo, aidha unaweza kuningoja hadi nirudi safarini ndio tuzungumze ana kwa ana kuhusu jambo hilo, kwa sasa siwezi kukwambia kama sina mimba ama ninayo,” alisema Odama.
Na Ally Katalambula

No comments

Powered by Blogger.