ad

ad

Buswita Aanza Mikwara Yanga

Kiungo wa ti,mu ya Yanga Pius Buswita.
BAADA ya kufunga bao lake la pili tangu atue Yanga, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo amewaambia mashabiki wa timu hiyo: “Tulieni, mbona mtafurahi sana.” Kauli hiyo, aliitoa wikiendi iliyopita mara baada ya kuifungia timu yake bao la kuongoza akipokea pasi ya Mrundi, Amissi Tambwe wakati Yanga ilipovaana na Reha FC katika mechi ya Kombe la FA iliyochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

Kiungo huyo, hilo ni bao lake la pili kulifunga tangu ametua kuichezea Yanga kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara akitokea Mbao FC ya Mwanza. Akizungumza na Championi Jumatano, Buswita alisema anafahamu mashabiki wa Yanga wanapenda kumuona akionyesha kiwango cha juu zaidi ya hicho amekionyesha kwa kifupi, hivyo ameomba muda kidogo.

Buswita alisema, ana mfupi tangu ametua kuichezea Yanga, hivyo kikubwa mashabiki wamvumilie huku akiendelea kuwathibitishia ubora wake taratibu kwenye mechi zijazo za ligi kuu na mashindano mengine. “Kikubwa watu wanatakiwa wafahamu kuwa, mimi nimetoka kwenye timu ndogo ya Mbao na nimekuja kwenye timu kubwa ya Yanga yenye presha kubwa ya mashabiki.

“Hivyo, ni lazima nibadilike taratibu kutoka mfumo niliokuwa nautumia nikiwa na Mbao na kuuchukua huu wa Yanga, hivyo siyo kazi ndogo inayohitaji muda kidogo wa mimi kuushika, pia kuzoeana na wenzangu. “Niwaahidi Wanayanga kuwa, mtafurahi na kunielewa wenyewe, kwani ninaamini uwezo wangu wa ndani ya uwanja ikiwemo kufunga na kutengeneza nafasi za kufunga mabao,” alisema.

No comments

Powered by Blogger.