ad

ad

Wakili wa Mobeto Afunguka, Asema Kesi Ipo Palepale


 Mwanamitindo Hamisa Mobeto
Muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, upande wa watoto kuitupilia mbali kesi ya kukataa kutoa matunzo ya mtoto inayomkabili msanii wa muziki wa kizazi kipya, aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto, wakili wa upande wa mashtaka, Walter Goodluck amefunguka na kueleza kila kitu kuhusu kesi hiyo huku akisisitiza kwamba kesi ipo palepale.

Akizungumza na mtandao huu, Wakili Walter kutoka Kampuni ya Century Attorneys alisema watu wengi wanachanganya taarifa kuhusu kesi hiyo lakini ukweli ni kwamba kesi ya msingi ipo palepale na kwamba kulitokea tatizo dogo la kiufundi kwenye hati ya awali ya mashtaka, iliyosababisha pingamizi la upande wa mshtakiwa kupita.

“Kesi ya msingi ni baba kukataa kutoa matunzo ya mtoto, kilichotokea ni kwamba sekretari wetu alifanya makosa madogo ya kibinadamu wakati akichapa maelezo yetu ya msingi na ndiyo maana walipoweka pingamizi, mahakama ikawapa wao ushindi.
Wakili Walter Goodluck
“Hata hivyo, hilo halibadilishi chochote kwa sababu kama nilivyosema, kesi ya msingi ipo palepale na jana baada ya mahakama kuifuta kesi, haraka tulirekebisha makosa yaliyotokea kisha tukaifungua upya ikiwa na marekebisho, kwa hiyo tunachosubiri sasa ni kupangwa kwa tarehe mpya ya kusikilizwa kwa kesi hiyo,” alisema Wakili Walter.

Alipoulizwa kama kiwango kinachoombwa na Mobeto kinaendana na sheria iliyopo, Wakili Walter alifunguka kwamba watu wengi hawajui sheria na ndiyo maana wapo wanaosema kwamba kiwango anachotakiwa kupewa ni kikubwa sana.

“Kwa kawaida, Sheria ya Haki za Mtoto ya Mwaka 2009 inaangalia uwezo na kipato cha baba kwa sababu hata katika maisha ya kawaida, uwezo wa baba ndiyo unaotoa tafsiri ya watoto watakula nini, kama baba anao uwezo, watoto wanaweza kuwa wanakula nyama hata kila siku. Kiwango hicho kinaendana na kipato cha baba yake.

“Kwa kawaida haya mapingamizi huwa yanawekwa kwa ajili ya kupoteza muda tu na kwa kawaida, kesi za namna hii huwa hazichukui zaidi ya miezi sita, kwa hiyo ni suala la muda tu.
Na Hashim Aziz/ GPL

No comments

Powered by Blogger.