ad

ad

Real Madrid Yatenga Euro Milioni 200 Kumnasa Neymar

Mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata 
WAKATI wengi wakiamini ni ngumu kwa Real Madrid kumsajili nyota wa PSG, Neymar, mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata amesema Madrid huwa haishindwi kitu, hivyo inaweza kumsajili mchezaji huyo.
Morata ambaye ni nyota wa zamani wa Madrid, amesema kuna ugumu wa usajili huo kutekelezeka lakini historia ya timu yake hiyo ya zamani inawapa wepesi wa kumsajili Neymar.
Nyota wa PSG, Neymar
Neymar raia wa Brazil amekuwa akihusishwa kujiunga na Madrid ikiwa ni miezi michache tangu alipojiunga na PSG ya Ufaransa akitokea Barcelona ya Hispania. Nahodha wa Madrid, Sergio Ramos hivi karibuni amenukuliwa akisema milango ipo wazi kwa Neymar, 25, kujiunga nao.
Neymar ambaye aliweka rekodi ya dunia aliposajiliwa kwenda PSG kwa dau la pauni milioni 198, Agosti mwaka huu, hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao 11 katika mechi 12 alizocheza za michuano yote.
Morata akizungumzia tetesi hizo za usajili wa Neymar kwenda Madrid, alisema: "Ni ngumu Neymar kwenda Madrid kutokana na mambo ya huko nyuma, huyu amecheza Barcelona.
"Lakini tayari tumeona jinsi kila kitu kinavyowezekana kwa Madrid, hivyo naamini Madrid ikiamua inaweza kumsajili Neymar na kila mmoja wetu akashangaa. “Madrid wakitaka kufanya jambo, hakuna anayeweza kuzuia, hivyo kama wana nia ya kweli, basi wanaweza kumsajili Neymar.”
Madrid inataka kukiongezea nguvu kikosi chake kinachonolewa na Zinedine Zidane kwani hadi sasa kina pointi nane nyuma ya Barcelona katika msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ katika mechi 11

No comments

Powered by Blogger.