ad

ad

Mpira wa Kombe la Dunia 2018 wazinduliwa


KAMPUNI ya vifaa vya michezo ya Adidas, imeutambulisha mpira wa Telstar 18 utakaotumika katika michuano ya Kombe la Dunia 2018 huko Urusi.

Mpira huo rudio la toleo lake lililotolewa kwa mara ya kwanza mwaka 1968 katika Kombe la Ulaya Italia halafu mara ya pili mwaka 1974 katika Kombe la Dunia huko Ujerumani Magharibi.

Adidas imeongeza utaalamu wa hali ya juu katika mpira huo kwa kuweka alama zitakazowawezesha watazamaji kuuona kwa mbali kwa kutumia simu zao za kisasa.

Mmoja kati ya mastaa walioujaribu na kuukubali mpira huo ni nyota wa Barcelona na Argentina, Lionel Messi ambaye alisema; "Nimepata bahati ya kuujaribu mpira huu, ni mzuri sana.

“Una umbo zuri jipya, rangi nzuri na kila kitu chake kinavutia.” Mkuu wa Bidhaa za Soka wa Adidas, Roland Rommler alisema Telstar 18 unawaletea changamoto mpya katika uzalishaji wao kwani ni bora kwa mipira iliyopo sokoni sasa.

“Huu ni mpira bora kwa matumizi ya sasa, ilifanyika kazi ngumu ya kuundeleza mpira wa zamani wa Telstar huku tukiweka teknolojia ya sasa,” alisema Rommler. Michuano ya Kombe la Dunia 2018, itaanza Alhamisi ya Juni 14 na itamalizika Jumapili ya Julai 15, mwakani.

No comments

Powered by Blogger.