Ndoa Ya Shilole Haina Mwaliko, Kufunga Ndoa Desemba
Zuwena Mohamed ‘ Shilole’ Ashirafu Uchebe.MWA NAMUZIKI mahiri wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed ‘ Shilole’ amesema kuwa anatarajia kufunga ndoa yake Desemba, mwaka huu na mpenzi wake Ashirafu Uchebe, lakini sherehe ya ndoa wataifanyia sehemu ya wazi ili kila mtu ahudhurie, hivyo itakuwa haina kadi ya mwaliko.
Zuwena Mohamed ‘ Shilole’ akiwa na mpenzi wakeShilole ameiambia Kilinge k u w a anamshukuru Mungu, mpenzi wake huyo ameshatoa mahari kubwa nyumbani kwao, kwa hiyo kilichobaki sasa hivi ni ndoa tu na haitakuwa ya kuhudhuriwa na watu maalumu kama wanavyofanya wengine, bali k ila mmoja anaweza kuishuhudia.“Ndoa yangu sitafanya ya siri kama wanavyofanya watu wengine, nitafanya sehemu ya wazi kabisa na wala haitakuwa na kiingilio hata kidogo, maana napenda ionwe na watu wote na washuhudie kila kin a c hoe ndelea,” alisema Shilole.

Post a Comment