Jokate Awapiga Pini Wanafunzi Kuingia Gesti
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ akiongea na wanafunzi Shule Ya Sekondari Mugabe (hawapo pichani) iliyoko Sinza A, Wilaya ya Ubungo Kama Mgeni Rasmi wa Mahafali ya 9 ya Kidato Cha Nne na kuweza kujionea shughuli mbali mbali za kitaaluma na kuongea na wanafunzi, walimu na wazazi/walezi juu ya changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao.[/caption]MWANAMITINDO ambaye pia ni Kaimu Katibu Hamasa na Chipukizi wa UVCCM, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amewapiga pini wanafunzi wa Mugabe Sekondari kuingia nyumba za kulala wageni ‘gesti’ ambazo zimewazunguka eneo hilo. Jokate aliwapiga pini wanafunzi hao kwenye hotuba yake alipokwenda kwenye mahafali ambapo alikuwa ni mgeni rasmi na kuahidi kuwajengea fensi ‘ukuta’ ili kukwepa usumbufu uliopo kwa sasa ambapo mbali na mazingira kuwa magumu lakini pia kelele za hapa na pale kwani kuna nyumba za kulala wageni pamoja na baa mbalimbali.
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ akifanya yake na wanafunzi haoJokate alienda mbali zaidi kwa kutoa agizo kwamba gesti zote na baa zilizopo Sinza, Dar zisiwaruhusu wanafunzi kuingia hasa wale wa Shule ya Sekondari Mugabe.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, Jokate alisema alisukumwa na changamoto zinazowakabili wanafunzi hao kwani mbali na kelele nyingi pia kuna baa na gesti nyingi zinazozunguka eneo hilo.
“Nimesema gesti zote zinazozunguka eneo la shule ya Mugabe wasiruhusu wanafunzi kuingia, ukuta utaanza kujengwa wanafunzi wakifunga shule ili waweze kupata utulivu wakati wa kusoma kwao kwa kuwa kwa sasa hawana amani kabisa,” alisema Jokate.
Post a Comment