Kaburi La Ivan Ssemmwanga Lafukuliwa Uganda
POLISI wilayani Kayunda nchini Uganda inawatafuta watu waliojaribu kulifukua kaburi la marehemu Ivan Ssemwanga lililoko katika kijiji cha Nakaliro usiku wa Jumanne iliyopita ili kuutoa mwili wake. Ssemwanga alizikwa kijijini kwao huko Mei mwaka huu katika mazishi yaliyokuwa na shamrashamra kibao.
Shimo kubwa kwenye kburi la Ivan.
Kaburi la Ivan lilivyofukuliwa.
Kaburi lilivyofukuliwa.
“Tumekuwa tukisikia uvumi kwamba waganga walikuwa wanalitaka fuvu la Ssemwanga ili walitumie kuwapa utajiri wateja wao wawe matajiri kama alivyokuwa Ssemwanga,” aliongeza Wamala. Watu waliojaribu kulichimbua kaburi hilo dhahiri walishindwa kulitoboa kutokana na ugumu wa zege lililochanganywa na nondo.
Kaburi la Ivan likiwa na limetapakaa noti.
Tangu kuzikwa kwa Ssemwanga, ndugu zake walikodi walinzi kulinda kaburi hilo lakini habari za kuaminika zimesema walishindwa kuwalipa mishahara yao kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa. Inasemekana walinzi hao mwezi wa kwanza walilipwa Sh. 600,000 mbali na kwamba walikuwa wamekubaliana kuwalipa Sh. milioni moja.
Post a Comment