Zari Anunua Benz E-Class Kumfunika Hamisa Mobeto (Video)
TUJIUNGE NA CHANZO Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na mjasiriamali huyo, Zari alichukizwa zaidi baada ya Mbongo Fleva huyo kusema amejitolea Rav 4 hiyo kwa ajili ya kumuwezesha Mobeto katika suala zima la kliniki ya mtoto wake. SUBSCRIBE: https://www.youtube.com/c/KidaniStars
“Ujue Zari alipoona watu wanazungumza sana juu Mobeto kupewa gari hilo na kumshushia vijembe mitandaoni, alichukia sana kwa maneno yale na kuahidi kuwaziba mdomo mashabiki wote wanaomsapoti Mobeto ndiyo akaamua kuongeza listi ya magari yake ya kifahari kuonesha kwamba Rav 4 si chochote, si lolote,” kilisema chanzo. SUBSCRIBE: https://www.youtube.com/c/KidaniStars GARI HILI HAPA Chanzo kilizidi kutiririka kuwa, kabla ya sherehe yake ya kuzaliwa, Zari aliamua kununua ndinga hilo aina ya Mercedes Benz E-Class (E250 CDI AMG Sport), model 2013, CC 2143. “Gari hilo limekuwa miongoni mwa magari yake ya kifahari na tayari ameliandika jina lake (Zari 3 GP). Si mnajua kuwa baada ya mumewe kufariki alipewa uongozi mkuu katika Chuo cha Brooklyn, kwa sasa huko ndiyo huwa anaenda nalo.” SUBSCRIBE: https://www.youtube.com/c/KidaniStars SUBSCRIBE: https://www.youtube.com/c/KidaniStars SUBSCRIBE: https://www.youtube.com/c/KidaniStars
FULL MBWEMBWE MITANDAONI Mapema baada ya kununua ndinga hilo, Zari kupitia ukurasa wake wa Snapchat, aliliweka na kuandika maneno; ‘welcome home baby’ akimaanisha kuwa analikaribisha ndinga hilo katika himaya yake mpya huko Sauz.
KIKUBWA NI HESHIMA
Chanzo kiliendelea kumwaga ubuyu kuwa, Zari ameamua kufanya yote hayo kwa ajili ya kujijengea heshima ambayo imeonekana kama kuyumba baada ya watu kumsema kwamba hana utajiri, anabebwa tu na msanii wake wa Bongo Fleva.
“Miongoni mwa vitu ambavyo Zari havipendi ni kushushiwa heshima, sawa alikubali kumsamehe mtu wake baada ya kusalitiwa lakini hakufurahishwa na maneno ya watu mitandaoni.
“Benz aliyoinunua ina thamani ya dola za Uganda milioni 442 (zaidi ya milioni 269 za Kitanzania) na yote hii ameifanya kwa lengo la kumfanyia kufuru Hamisa aliyekuwa amezawadiwa Rav 4 ya thamani ya shilingi milioni 25,” kilisema chanzo hicho.
Post a Comment