Taifa Stars ijitahidi basi ili mashabiki wajazane uwanjani
MOJA ya changamoto inayopitia timu yetu ya Taifa, Taifa Stars ni kitendo cha mashabiki wachache kujitokeza kuangalia mechi zao uwanjani. Si jambo dogo hata kidogo na hili limekuja baada ya timu hiyo kuwa na matokeo mabaya kwa muda mrefu kidogo.
Pamoja na kuwa na matokeo mabaya ila inakosa watu wa kushawishi mashabiki waweze kujitokeza viwanjani. Nakumbuka enzi za Kocha Mbrazili, Marcio Maximo siku Taifa Stars ikicheza mashabiki lukuki walikuwa wakienda uwanjani kuishangilia na siyo uwanjani tu hata mitaani hadithi zilikuwa hizo tu. Lakini hivi sasa hilo jambo halipo tena na sijui mashabiki wamesusa nini lakini nadhani kama nilivyosema hapo juu kwa sababu ya matokeo mabaya.
Nchi za wenzetu timu zao za taifa zikicheza kila kona hadithi ni hiyo na uwanjani wanajazana kwelikweli. Pamoja na timu ya sasa kuwa na matokeo mazuri chini ya Kocha Salum Mayanga, lakini bado mashabiki wamegoma maana ni wachache mno wanaojitokeza kuangalia mechi zake na hapo ndiyo utajiuliza kuna nini jamani. Mwenyewe Mayanga anasema hivi sasa anajenga timu na ipo siku Watanzania wataikubali Taifa Stars na mimi naliombea heri hilo. Kikubwa ni matokeo mazuri tu ya ndani ya uwanja na hilo ndilo Watanzania hasa wapenda soka wanalipenda.
Kikubwa jamani Watanzania tumechoka kuona wenzetu timu zao zikifanya vizuri na sisi tukilia na kutoa machozi na kujipa moyo kuwa labda mwaka f’lani na sisi tutaweza na hilo ndilo linalochosha jamani. Leo tunacheza na Malawi tunachotaka ni ushindi ili mjiweke kwenye nafasi nzuri kwenye viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na baada ya hapo mje kufanya vizuri kwenye michuano ya kufuzu Kombe la Afrika na hapo ndipo kwenye ugonjwa wetu mkubwa.
Mara ya mwisho Tanzania kushiriki michuano ya Afrika ilikuwa mwaka 1980 sasa sijui Mayanga na mwenzie wataweza? Maana tumechoka kuwa wasindikizaji hilo halina siri hata kidogo. Tunataka kuona Taifa Stars ikifuzu kwa michuano mikubwa kama Afcon siyo kuishia kwenye Cecafa tu na Cosafa, najua ikifikia kwenye hatua hiyo haitakuwa na haja ya kupiga kelele za mashabiki kwenye kuishangilia uwanjani wenyewe watakuja. Sasa kazi kwenu kwa TFF, benchi la Taifa Stars na wachezaji wenyewe na huo ndio mtihani kwenu mkubwa mkiweza tu basi tutakuja na tunawatakia kila lenye heri.

Post a Comment