Nassari ampa onyo kali Gambo Kisa Wagombea
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ametoa onyo kwa viongozi wa
Serikali ya Arusha, akiwepo Mkuu wa Mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru kwamba waache kuwatishia wagombea wa chama chake (CHADEMA)
ikiwepo kuwashawishi waajiondoe
kwenye uchaguzi wa madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 26.
Mh. Nassari amewaonya viongozi hao huku
akiwakumbusha kwamba wanatakiwa wafahamu wana-deal na watu wa aina gani
huku akiwakumbusha kwamba kama wanataka kurekodiwa.
"Onyo kwa RC na DC! acheni
kuwatisha wagombea wetu, acheni kuwatuma watu wakiwemo viongozi wa dini
kuwashawishi wajiondoe kwa ahadi zilezile. Mmesahau mna-deal na watu wa
aina gani?? Au bado mnataka kurekodiwa??" Ameandika Nassari katika mtandao wake wa Facebook.
Ameongeza kwamba "We are determined, (Tumedhamiria) Tukutane kwa debe!!"
Mapema mwezi huu Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) ilitangaza kwamba uchaguzi mdogo wa marudio wa madiwani
katika kata 43 utafanyika Novemba 26 mwaka huu, huku Arusha ikiwa
imepoteza kata kumi.
Post a Comment