Mwana: Ndoa Haitoniachisha Kuigiza Bongi Muvi
Akibonga Mwana alisema kuigiza ni kitu ambacho kiko kwenye damu na tangu akiwa mtoto alikuwa anatamani kazi hiyo hivyo alipokuwa mkubwa alifanikiwa kusomea kazi nyingine lakini hakuzifanyia kazi hata kidogo, akaamua kuingia kwenye filamu na amekuwa akiyafurahia maisha kwa kuwa anafanya kazi anayoipenda.
“Siwezi kuacha kuigiza kamwe hata siku nitakayojaaliwa kupata ndoa nitaendelea nayo tu huyo mwanaume atake asitake maana ndiyo kazi aliyonikuta nayo na siku zote kuacha kazi unayoipenda siyo kitu rahisi,” alisema Mwana
Post a Comment