Miaka Miwili ya Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp
KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amekamilisha miaka miwili kwenye kikosi hicho huku mashabiki wakimgawa kwenye makundi mawili.
Wengi wamekuwa wakisema kuwa kila alichokifanya kocha huyo kwenye timu hiyo siyo kile ambacho walikuwa wanakitaka huku wengine wakiamini kuwa ameshafanya kazi nzuri.
Liverpool wamekuwa wakitamani mara kwa mara kupata ubingwa wa Ligi Kuu England ambao hawajautwaa kwa miaka mingi lakini bado kocha huyo anaonekana kuwa hawezi hata kuwapa ubingwa huo msimu huu.
Kocha huyo alichukua nafasi ya kocha Brendan Rodgers Oktoba 8, mwaka 2015, huku akiwa aliwindwa na timu hiyo kwa muda mrefu sana.
Kocha huyo ambaye alipata mafanikio makubwa akiwa na Borussia Dortmund alipofika England aliahidi kutengeneza kikosi imara ambacho kinaweza kutwaa ubingwa wa England lakini kwa miaka miwili sasa bado mambo hayo hayajatimia.
Hata hivyo, Klopp pamoja na kufanya usajili kabambe kwa kipindi chake chote alichokaa kwenye timu hiyo, ameshindwa kufanya vizuri, huku Liverpool wakifurahia nafasi ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya tu.
Lakini kwa kipindi hicho kuna mambo mengi ambayo yamebadilishwa na kocha huyo kwenye kikosi cha Liverpool baadhi ni:
USAJILI KABAMBE
Liverpool wamekuwa wakifanya usajili mkubwa kwa kipindi chote ambacho kocha huyo amekaa hapo.
Lakini bado hakuna mambo makubwa ambayo wameweza kuyafanya hadi sasa, huku wengi wakionekana kutokuwa na kiwango kile ambacho kilikuwa kinategemewa.
Pamoja na kusajili wengi, lakini Sadio Mane aliyesajiliwa kwa pauni milioni 30, ndiye msaada pekee kwenye timu hiyo kwa sasa huku akifuatiwa na Gini Wijnaldum ambaye alitua hapo akitokea Newcastle.
Pia Mo Salah, aliyeingia hivi karibuni tayari ameshaonyesha makucha yake kwa kiwango alichoonyesha kwenye michezo michache tangu ajiunge na timu hiyo.
Lakini pamoja na hivyo bado kocha huyo ameonekana kuwa na safu mbovu ya ulinzi tangu ameanza kuitumikia timu hiyo.
AINA YA KUCHEZA
Klopp ametumia nguvu kuwa kuhakikisha timu hiyo inacheza soka safi lakini pia inapata matokeo mazuri.
Liverpool imekuwa ikionyesha soka la kuvutia kwa kipindi kirefu chini yake na hapo ndiyo imeweza tena kurudisha imani yake kuwa inaweza kupambana na timu kubwa za England, Man United, Man City na hata Chelsea na kuaminika kuwa inaweza kupata ushindi.
Klopp amekuwa akiwasajili wachezaji ambao wana uwezo mkubwa sana wa kuuchezea mpira wakiwemo Mane, Salah, Roberto Firmino na Philippe Coutinho.
Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya soka wamekuwa wakiponda aina ya usajili wa Klopp kwa kuamini kuwa kocha huyo amekuwa akishindwa kusajili mabeki wazuri tangu alipojiunga na timu hiyo.
MASHABIKI
Mashabiki wa Liverpool wamekuwa na imani kubwa juu ya kocha huyo na wamekuwa wakifurahia kila hatua kwenye timu hiyo huku wakiongezeka kwa wingi sana kwenye michezo michache ya hivi karibuni.
MAFANIKIO MSIMU HUU
Japo ni mwanzo wa msimu lakini Liverpool hawajaonyesha kiwango cha juu sana, wakiwa wanaonekana kuwa na safu mbovu ya ulinzi.
Liverpool tayari wameshapoteza mchezo mmoja na wametoka sare mitatu kati ya saba ambayo wameshacheza hadi sasa matokeo ambayo yanaonekana kutokuwa mazuri sana kwao.
Hata hivyo, timu hiyo inatajwa kuwa kati ya zile ambazo zinaweza kutinga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
MAFANIKIO YA KLOPP
Kwa Liverpool hana mafanikio makubwa sana akiwa hajatwaa ubingwa wowote, lakini kwenye kikosi cha Dortmund amekuwa na mafanikio mazuri akiwa alitwaa ubingwa wa Bundesliga mwaka 2010–11 na 2011–12.
Lakini pia akiwa hapo alitwaa ubingwa wa DFB-Pokal pamoja na DFL-Supercup.
Katika michezo aliyofundisha akiwa na Mainz, timu yake ya kwanza kubwa alifundisha michezo 270, alishinda michezo 109, alitoka sare michezo 78 na kufungwa michezo 83.
Akiwa Dortmund kocha huyo alifundisha michezo 318, alishinda 179, alitoka sare 69 na kupoteza michezo 70.
Hata hivyo akiwa Liverpool kocha huyo ameshafundisha michezo 111, ameshinda 55, ametoka sare michezo 33 na kufungwa 23.

Post a Comment