Kesi ya Masogange yapigwa kalenda tena!
DAR ES SALAAM: Kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili muuza nyago kwenye video za wasanii wa Kibongo, Agness Gerald ‘Masogange’, imepigwa kalenda tena ambapo ushahidi utatolewa Novemba 14, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar.
Mshitakiwa huyo alipaswa kuanza kujitetea jana, Alhamisi, lakini Wakili wa Serikali, Adolf Mkini aliomba kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ipangiwe tarehe nyingine. Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Mashauri aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 14, mwaka huu.
Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya Hakimu Mashauri kumuona mshitakiwa huyo kuwa ana kesi ya kujibu na kwamba anapaswa kujitetea na kuwaita mashahidi wake. Masogange anatetewa na mawakili, Nehemia Nkoko na Ruben Simwanza.
Kesi hiyo inaendeshwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula ambaye kwa upande wao kuwaita mashahidi watatu wa upande wa mashitaka kutoa ushahidi wao na kuufunga. Masogange anakabiliwa na mashitaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.
Pia mrembo huyo anadaiwa kufanya makosa hayo chini ya kifungu cha 18 (a) cha Sheria ya Kupambana na Dawa za Kulevya namba 5 ya mwaka 2015.
Post a Comment