JPM Afanya Mabadiliko Baraza la Mawaziri, Shonza Ndani, Kashilila Out
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri nchini huku akizigawanya baadhi ya wizara zikiwemo Wizara ya Kilimo na Mifugo, Nishati na Madini na kuongeza wizara mpya mbili na kufikisha jumla ya wizara 21. Katika Mabadiliko hayo, Mawaziri wawili na manaibu waziri wameongezwa. Aidha Rais Magufuli ametangaza mabadiliko na kuteua Katibu mpya wa Bunge huku akieleza kuwa aliyekuwa Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila atapangiwa kazi nyingine. ORODHA. Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu: Naibu Waziri – Stella Alex Ikupa Wizara ya Mifugo na Uvuvi: Waziri – Luhaga Mpina, Naibu Waziri -Abdallah Hamisi Ulega. Wizara ya Maji na Umwagiliaj: Waziri- Mhandisi Isack Kamwelwe, Naibu Waziri – Jumaa Hamidu Aweso. Wizara ya Nishati: Waziri – Dk. Medard Kalemani, Naibu Waziri – Subira Khamis Mgalu.
Wizara ya Madini: Waziri – Angellah Kairuki, Naibu Waziri -Stanslaus Haroon Nyongo. Wizara ya Maliasili na Utalii: Waziri – Hamis Kigwanhalla, Naibu Waziri – Japhet Ngailonga Hasunga. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji: Waziri –Viwanda/biashara – Dkt. Charles Mwijage, Naibu Waziri – Mhandisi Stella Manyanya. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia : Waziri – Prof. Joyce Ndalichako, Naibu Waziri -William Ole Nasha. Wizara ya Fedha na Mipango: Waiziri – Dr Philip Mpango, Naibu Waziri – Dr Ashatu Kijaji. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto: Waziri – Dkt. Ummy Mwalimu, Naibu Waziri, Dkt. Faustine Ndugulile. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo: Waziri – Dkt. Harrison Mwakyembe, Naibu – Juliana Daniel Shonza.
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji: Naibu Waziri – Mhandisi Stella Manyanya. Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI): Waziri – Selemani Said Jaffo, Manaibu Waziri – Peter Sekamba na Kakunda. Wizara ya Katiba na Sheria; Waziri – Prof. Palamagamba Aidan Kabudi. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi: Waziri – Mwigulu Nchemba, naibu Waziri- Eng. Hamad Masauni. Wizara ya Kilimo: Waziri – Dk. Charles Tizeba, Naibu Waziri – Mary Machuche Mwanjelwa. Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano: Waziri- januari Makamba, naibu Waziri – Kangi Lugola. Wizara ya Ulinzi nha Jeshi la Kujenga Taifa: Waziri – Hussein Mwinyi. Wizara ya Ardhi na Nyumba: Waziri- William Lukuvi, Naibu Waziri – Angelina Mabula. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano: Waziri – Prof. Makame Mbarawa, Naibu Waziri – Elias John Kwandikwa. Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, ameondolewa katika Baraza la Mawaziri lililotangazwa na Rais Maguful. Steven Kagaigai ameteuliwa kuwa Katibu wa Bunge na aliyekuwepo, Dkt. Thomas Kashililah atapangiwa kazi nyingine. Rais amesema kuwa, wote walioteuliwa watakaoridhia uteuzi wao, wataapisha Jumatatu ijayo, Oktoba 9, saa 3 asubuhi, Ikulu Dar es Salaam.
VIDEO YA RASI MAGUFULI AKITANGAZA MAWAZIRI
Post a Comment