ad

ad

BEKI YANGA ASEMA “SIMBA WANGETUFUNGA, HALI INGEKUWA MBAYA ZAIDI



Mara baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 kati ya Yanga dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Uhuru, Jumamosi jijini Dar Salaam, beki wa Yanga,

Gadiel Michael ameuzungumzia mchezo huo.

Gadiel ambaye alishiriki katika kipute hicho cha Ligi Kuu ya Vodacom amesema kuwa kama Simba wangewafunga baso hali ingekuwa mbaya kwao, lakini kwa kuwa wamepata sare anaona ni matokeo mazuri kwa pande zote na wanajipanga kwa ajili ya mchezo ujao.

Beki huyo wa zamani wa Azam FC, amesema kuwa wao walipata nafasi kadhaa ndogondogo lakini wakashindwa kutumia vizuri, hivyo kitendo cha Simba kutangulia kupata bao kiliwafanya wakaongeza nguvu zaidi.

“Matokeo siyo mazuri, nia yetu ilikuwa ni ushindi lakini kwa kuwa imekuwa sare, siyo mbaya sana, tunajipanga kwa ajili ya mchezo ujao,” alisema Gadiel.

No comments

Powered by Blogger.