Yanayoweza kumfanya mumeo atembee na mashosti wako
NI wiki nyingine tena tunakutana kupitia safu hii nakiamini muwazima
na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku kama kawaida. Mimi
nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwani amekuwa akiniongoza katika
kila ninalolifanya katika maisha yangu.
Ndugu zangu, maisha ya
kimapenzi yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana kwani kuna changamoto
nyingi zinazoweza kujitokeza kiasi kwamba usipoangalia unaweza kuishia
kusema hutakuja kumpenda mtu, heri uishi peke yako!
Tatizo kubwa ambalo limekuwa likiwasumbua wengi walio kwenye ndoa na
wale walio kwenye uhusiano wa kawaida ni usaliti. Uaminifu umepungua kwa
kiasi kikubwa, mke wa mtu kutembea na rafiki wa mumewe si kitu cha
ajabu siku hizi, mume wa mtu kutembea na mpangaji mwenzake siyo ishu.
Nashindwa kuelewa tunaelekea wapi.
Yaani imefika hatua ya mume wa mtu
kutembea na ‘hausigeli’ wake tena anafanya hivyo kwenye kitanda
anacholala na mkewe, hii si laana jamani? Usiulize kwa nini nimetoa
mfano huu, hili limetokea juzi tu kwa mtu wangu wa karibu sana. Alitoka
safari na aliporejea usiku akamfumania mumewe akiburudika na
‘hausigeli’, eti mwisho wa siku mwanaume anaomba asamehewe akidai ni
shetani kampitia.
Anyway nimeona nianze na hilo ambalo lina uhusiano wa kile
ninachotaka kukizungumzia leo. Kama nilivyotangulia kusema hapo mwanzo,
imekuwa si jambo la ajabu kusikia mume wa mtu katembea na rafiki wa mke
wake.
Wewe utakuwa ni shahidi wa hiki ninachokizungumza kwani kama hakijakutokea basi rafiki yako au ndugu yako kimempata.
Lakini
katika uchunguzi wangu nimebaini baadhi ya wake za watu wamekuwa
wakitengeneza mazingira ya waume zao kutembea na marafiki zao.
Unaweza kushituka kusikia hivyo lakini ndiyo ukweli wenyewe na utakubaliana na mimi baada ya kusoma vipengele vifuatavyo.
Ukaribu wa mume na marafiki wa mke
Kuna baadhi ya wanawake
wamekuwa na tabia ya kuwaweka waume zao karibu sana na marafiki zao.
Unakuta mwanamke eti anamruhusu mumewe kwenda klabu au baa na shosti
wake. Katika mazingira hayo unatarajia nini?
Sisemi uanze kumfikiria
tofauti rafiki yako lakini unachotakiwa kujua ni kwamba, sasa hivi kuna
wasichana micharuko ambao ukiwapa nafasi kidogo tu kwa mumeo
wanakupindua.
Kwa maana hiyo kitendo cha kumuweka mumeo karibu na mashosti wako
unatengeneza mazingira ya kusalitiwa kwa kujitakia hivyo unatakiwa kuwa
makini na watu ambao wanastahili kuwa karibu na laazizi wako.
Mawasiliano ya mume na marafiki wa mke
Sisemi marafiki zako
wasiwasiliane kabisa na mumeo lakini unatakiwa kuangalia wanawasiliana
kwa mambo gani? Utakuwa ni mtu wa ajabu kama utakubali mumeo apigiwe
simu au achati na marafiki zako halafu hakuna cha maana wanachoongea,
walahi utaula wa chuya!
Unatakiwa kuwa mkali pale unapoona mumeo
anawasiliana sana na marafiki zako wa kike kwani waliosalitiwa walianza
kuchukulia poa mazingira kama hayo mwishowe wakalia.
Mke kuanika siri za mumewe
Lingine ni tabia ya baadhi ya wanawake
kuwasimulia mashosti wao siri ambazo hawastahili kuzitoa nje. Kuna
wanawake sijui nisema ni ulimbukeni au ushamba!
Eti unamkuta mke
anasimulia mashosti wake jinsi mumewe anavyompa furaha wanapokuwa
faragha. Unajiuliza ni kwa nini mtu anafikia hatua hiyo.
Kimsingi
hili ni kosa kubwa linalofanywa na baadhi ya wanawake na kujikuta
wakikaribisha usumbufu kwa waume zao kutoka kwa wanawake micharuko.
Mwanamke kutochukua nafasi yake
Kwa kifupi mwanamke kushindwa kumdatisha mumewe ni kumfanya aangalie wapi kwingine anakoweza kupatiwa kile anachokihitaji.
Hili
liwe fundisho kwa wanawake waliobahatika kuingia kwenye maisha ya ndoa.
Kumridhisha mumeo ni kumfanya aepukane na vishawishi vinavyoweza
kumfanya akusaliti.
Mpe mapenzi atosheke asifikiria kukusaliti, mpe kila anachokitaka
kutoka kwako (ila usimruhusu kuruka ukuta). Hii itamfanya asiwe na tamaa
ya kupoteza muda wake kwa marafiki zako ambao ni micharuko wanaotamani
kuonja asali yako.
Post a Comment