WEMA ALA KIAPO CHA KUZAA NA IDRIS

Baada ya msanii ‘classic’ katika fani ya uigizaji Bongo, Wema Sepetu kurejesha majeshi kwa Mchekeshaji Idris Sultan, mwanadada huyo amekula kiapo cha kuzaa na jamaa huyo. Wema na Idris walizua gumzo wikiendi iliyopita ndani ya Ukumbi wa Cinemax, Mlimani City jijini Dar katika uzinduzi wa filamu mpya ya mrembo huyo iliyokwenda kwa jina la Heaven Sent.
Mara baada ya uzinduzi huo, Wema aliweka picha na ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram na kuonesha kwamba anatamani kuitwa mama na hana kipangamizi kumfanya Idris aitwe mama kupitia tumbo lake.
Mdada huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akililia kuitwa mama aliweka picha hiyo aliyoiedit na kuichanganya na picha ya mtoto aliyemlisha maneno akisema ‘I love love you mama...’ kisha yeye akaandika ‘This made me cry’ akionesha kuwa na hamu ya kuambiwa anapendwa na mwanaye.
Kufuatia maneno hayo ya mtandaoni, Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Wema na kumuuliza mpango wake huo wa kumzalia Idris ambaye aliwahi kumpa ujauzito kipindi cha nyuma kisha ukaharibika, alipopatikana alisema:
“Niko tayari kwani nini shida? Ikitokea kwa Idris itakuwa sawa tu, natamani kuwa mama,” alisema Wema.
Katika mahojiano mengine na Ijumaa, mrembo huyo aliweka wazi kuwa amempata daktari maalum wa kumuangalia mwenendo wake kuhakikisha suala lake la uzazi linakwenda vizuri.
“Nina dokta ambaye mara kwa mara anafuatilia mwenendo wangu kwani ameshalijua tatizo linalonisumbua na hivyo ananifuatilia kwa karibu kuhakikisha ninafanikiwa kuwa mama,” alisema Wema.
STORI: IMELDA MTEMA| IJUMAA
Post a Comment