Vodacom Wazindua ‘Pinduapindua’ Kwa Wateja Wajanja (Video)
Mkuu
wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Vodacom, Nandi Mwiyombella,
akiongea na wanahabari na wafanyakazi wa Vodacom wakati wa kuzindua
kampeni mpya ya Pindua Pindua makao makuu ya Vodacom jijini Dar.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, akifafanua tofauti ya huduma ya Pinduapindua na huduma nyingine za Vodacom.
Viongozi mbalimbali wa Vodacom wakiwa na mabango ya ujumbe tofauti wa Pinduapindua.
Wafanyakazi wa Vodacom wakicheza dansi ya Pinduapindua.
Kikundi cha Pinduapindua Dance kikionyesha uwezo wao wa kupindukapinduka.
Baadhi ya wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Vodacom wakifuatilia uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa Vodacom wakifanya yao.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao (katikati) akicheza dansi ya aina yake ya Pinduapindua.
Uzinduzi huo umefanyika makao makuu ya Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam.
Pinduapindua ni aina maalum ya vifurushi ambapo mteja anapata uniti zinazompa uhuru wa matumizi. Akiwa na Pinduapindua units anapata uhuru wa kuamua matumizi yake iwe kupiga simu, kuperuzi au kutuma sms kwa sababu matumizi ya uniti anajipangia mwenyewe. Pia PinduaPindua inakupa Facebook, WhatsApp na SMS bure.
Jinsi ya kujiunga na Pinduapindua: Piga *149*01# na chagua Pinduapindua na unaweza kumnunulia za Pinduapindua rafiki yako.
Mchanganuo wa gharama za Pinduapindua units
Dk 1 (Voda –Voda) = uniti 1
Dk 1 (Mitandao yote) = uniti 5
MB 1 = uniti 1 SMS 1 = uniti 1 (hii ni baada ya kumaliza SMS za BURE)








Post a Comment