Tambwe: Simba bila Okwi hakuna timu
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe,
amefurahishwa na matokeo ya bila kufungana ambayo Simba iliyapata juzi Jumamosi
ilipocheza na Azam FC. Hata hivyo, Tambwe ambaye msimu wa 2013/14 alikuwa
akiitumikia Simba, alisema kuwa alijua kabisa timu hiyo isingepata matokeo
mazuri katika mechi hiyo bila ya uwepo wa Mganda, Emmanuel Okwi kwenye mchezo
huo.
Akizungumza Tambwe alisema kuwa kwa washambuliaji
wa Simba waliopo hivi sasa, ukimwondoa Okwi, ilikuwa ni ngumu kwao kuifunga
Azam kutokana na kutokuwa na ubunifu wa kutafuta ushindi pindi wanapokuwa
wamebanwa vilivyo na mabeki wa timu pinzani.
“Matokeo hayo nimeyapokea vizuri na nimefurahi baada
ya kuona kile nilichokuwa nikiwaza akilini kwangu kimetimia, kwani nilijua
kabisa Simba wangekutana na matokeo hayo katika mchezo huo. “Hiyo ni kwa sababu
washambuliaji wengi wa timu hiyo siyo wabunifu wa kutafuta mbinu mbadala za
kufunga pindi wanapokuwa wamebanwa vilivyo na wapinzani wao.
“Mchezaji pekee
ambaye angeibeba Simba katika mechi hiyo alikuwa ni Okwi lakini baada ya
kusikia tu kuwa hatacheza mechi hiyo moja kwa moja matokeo hayo waliyopata
yakanijia akilini kwangu,” alisema Tambwe na kuongeza: “Kwa hivyo hivi sasa
dalili ya sisi kuchukua ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya nne mfululizo nimeanza
kuiona na ninamwomba Mungu nirejee mapema uwanjani ili niweze kuisaidia timu
yangu ya Yanga kutimiza ndoto yetu hiyo.”
Post a Comment