ad

ad

Rashford ni Mshambuliaji Hatari Manchester Utd

 M A N C H E S T E R United imeanza msimu vizuri, kumekuwa na matumaini makubwa kwa mashabiki wa timu hiyo kuwa timu yao itafanya vizuri kutokana na kuonekana kama imekamilika katika idara nyingi. 

Ushindani wa namba ni mkubwa kikosini hapo chi¬ni ya Kocha Jose Mourinho, pamoja na hivyo, chipukizi Marcus Rashford mwenye umri wa miaka 19 ameendelea kuthibitisha kuwa anao uwezo wa kushindania namba katika kikosi cha kwanza. 


Rashford amekuwa na mwendelezo mzuri wa kile anachoki¬fanya kutokana na kasi yake ya ufungaji, kuwasumbua wapinzani na jinsi ambavyo ameweza kuwa tish¬io hata kwa walinzi wakongwe. 


Usiku wa Jumanne ya wiki hii aliweka rekodi ya kipeke ya kufunga bao katika mechi yake ya kwanza kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Alifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya FC Basel ambapo United ilishinda kwa mabao 3-0. 


Bao moja alilofunga akitokea benchi katika mchezo huo limemfanya kuwa amefunga mabao katika mechi saba za kwanza za michuano ambayo amekuwa akianza. Yaani katika kila mechi ya kwanza ya michuano husika amekuwa akifunga. 


Tujikumbushe jinsi ambavyo Rashford amekuwa hatari katika michuano saba tofauti aliyopewa nafasi tangu mwaka 2016 ambapo hii inajumuisha klabu na timu ya taifa lake ya England. 


Rekodi yake hiyo inaonyesha amefunga katika kila mechi yake ya kwanza ya mi¬chuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Europa League, Premier League, League Cup, England timu ya wakubwa na England U21:
 

EUROPA LEAGUE
Man United v Midtjylland
Februari 25, 2016
Katika hii mechi h a k u w e m o k w e n y e
 ratiba ya kucheza lakini alilazimika kupangwa na Kocha Louis van Gaal baa¬da ya kuumia kwa Antony Martial wakati wa kupasha misuli. United ilipata ushindi wa mabao 5-1 na kufuzu katika Hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.
Alifunga mabao mawili na kuwafanya mashabiki wengi wa United kujiuliza juu ya mfungaji huyo kwa kuwa kocha alilaz¬imika kuwatumia chipukizi wengi katika mchezo huo uliopigwa Old Trafford kuto¬kana na kuwa majeruhi. 


PREMIER LEAGUE
Man United v Arsenal
Februari 28, 2016
Siku chache baadaye United ilikutana na Arsenal ambayo ilikuwa katika ubora mzuri huku wenyeji wakiwa na chipukizi wengi, ilionekana ni suala la Arsenal itashin¬da ngapi na siyo timu gani itashinda, lakini Rashford alibadili fikra za mamilioni ya mashabiki wa soka kwa kufunga mabao mawili na kuipa timu yake ushindi wa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Old Trafford. 


TIMU YA TAIFA
England v Australia
Mei 27, 2016
Alifanikiwa kufunga bao katika dakika ya tatu tu tangu aanze kuichezea timu ya wakubwa ya England, bao lake hilo lilichangia kuiwezesha Eng¬land kushinda 2-1 kwenye Uwanja wa Light. 


TIMU YA TAIFA
England U21 v Norway U21
Septemba 6, 2016
Kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 alimuomba Rashford kutokana na umuhimu wa mchezo huo, ‘dogo’ haku¬fanya makosa, kwani alifunga mabao matatu ‘hat-trick’ na kuchangia England kushinda 6-1 katika mchezo huo wa ku¬fuzu Euro 2017.


 Man United v North¬ampton
Septemba 21, 2016
United ikiwa ugenini ilishuhudiwa Rash¬ford akitokea benchi na kuipa timu yake ushindi katika mechi ya Kombe la Ligi, bao ambalo lilitokana na uzembe wa kipa wa wapinzani zikiwa zimesalia dakika 16 mchezo kumalizika, ambapo walishinda mabao 3-1. 


LIGI YA MABINGWA ULAYA
Man United v FC Basel
Septemba 12, 2017
Akiwa kwenye uwanja wake wa kujidai wa nyumbani, akitokea benchi pia, kija¬na alifunga bao katika dakika ya 77 aki¬malizia kazi nzuri ya Marouane Fellaini.
Rekodi zinaonyesha katika michuano yote ambayo amecheza, Rashford al¬ishindwa kufunga katika mchezo wake wa kwanza wa FA Cup tu, kwingine kote akianza lazima awasalimie kwanza.


No comments

Powered by Blogger.