Linah: Sioni shida kuolewa na Muislam!,Kufunga Ndoa Hivi Karibuni
Ijumaa: Wanamuziki wengi wamekuwa wakijishauri sana katika suala zima la kubeba ujauzito kutokana na kazi zao, wewe halikukuumiza kichwa hili?
Linah: Kwa sababu niliamua kwa moyo mmoja kabisa wala hilo sikujiuliza hata mara moja kwa kuwa nilitamani mtoto.

Ijumaa: Wakati unaelekea chumba cha kujifungua, muda mfupi kabla ya kuingia uliposti picha ukiwa kwenye uchungu, haikukuletea matatizo hasa kutokana na mila zetu?
Linah: Kwanza ile picha sijaiposti nafikiri kulikuwa na mtu pale hospitali na pia haikuwa siku ambayo najifungua ilikuwa ni siku ambayo nilienda kuonana na daktari, sikuwa najisikia vizuri.
Ijumaa: Baba watoto wako yeye sio staa?
Linah: Hapana wala hayuko huko kabisa.

Ijumaa: Sasa mnawezaje kuendana maana mastaa kuna mambo mengi?
Linah: Unajua huyu mchumba wangu alinipenda tangu 2009, ndio kwanza naanza kutoka lakini hakupata muda wa kunifikia hivyo anajua kazi yangu na ndio maana niko nae amekubali kila kitu changu.
Ijumaa: Vipi kuhusu ndoa wewe na mchumba wako kuna matarajio hayo?
Linah: Ndiyo ni hivi karibuni.
Ijumaa: Lakini mpenzi wako ni Muislam na ninajua wazi kuwa wewe umetoka kwenye familia ya Kikristo inakuaje hili?
Linah: Ni kweli ni Muislam lakini sioni shida kuolewa naye.
Ijumaa: Kipindi cha ujauzito uliweka picha za kuonesha tumbo wazi, hiyo haikuleta shida kwa wakwe zako?
Linah: Namshukuru sana Mungu, nimepata wakwe waelewa sana kikubwa wao wanataka heshima wala hilo la picha hawalitazami.
Ijumaa: Wewe na msanii Amini mlikuwa wapenzi mnaopendana sana, vipi mkikutana sasa hivi?
Linah: Mimi na Amini tunaheshimiana sana kwa kuwa tayari ana mke wake na mimi nina mtu wangu.
Ijumaa: Asante kwa ushirikiano wako
Post a Comment