ad

ad

Omog: Gyan ni Pacha wa Okwi

KOCHA Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, amesema straika wake mpya, Nicholaus Gyan, anafaa zaidi kucheza sambamba na Emmanuel Okwi kutokana na staili yake ya uchezaji. 
 
Gyan ambaye aliwasili juzi Jumamosi akitokea kwao Ghana, moja kwa moja ameungana na kikosi hicho kinachojiandaa na mechi yao ijayo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam itakayopigwa Jumamosi ya wiki hii.

Straika huyo aliyesaini mkataba wa miaka miwili akitokea Ebusua Dwarfs ya nyumbani kwao, mwanzoni mwa mwezi uliopita alitua nchini na kutambulishwa katika Tamasha la Simba Day, kisha akarudi kwao Ghana kumalizana na timu yake aliyokuwa akiitumikia. 

Akizungumza  Omog alisema, kwa jinsi alivyomuona siku ile kwenye Tamasha la Simba Day, amegundua kwamba anaweza kucheza vizuri zaidi akiwa na mtu mwenye kasi uwanjani kama Okwi.
 

“Gyan ana kasi na anajiamini sana kama ilivyo kwa Okwi, nilimuona mara moja kwenye Tamasha la Simba Day jinsi anavyocheza, hivyo akipata mtu mwenye kasi kama yeye, atakuwa msaada mkubwa sana kwetu. 


“Kwa sababu ameshakuja, hatuna budi kuliangalia hilo kwa sababu kama ujuavyo yeye ni mshambuliaji, ni lazima tumtumie zaidi katika kutupatia ushindi kwenye mechi zetu za ligi.

 “Kwa sasa hatutakuwa na shida kwenye safu yetu ya ushambuliaji kwani tutakuwa na wachezaji wengi katika nafasi hiyo, hivyo kilichobaki ni kuona tunashinda kila mchezo ulio mbele yetu,” alisema Omog

CHANZO: CHAMPIONI

No comments

Powered by Blogger.