MIEZI michache ikiwa imepita tangu mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni muuza nyago, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’
ahongwe gari aina ya Benzi, amekumbwa na aibu ya mwaka kufuatia kuporwa
na aliyekuwa mpenzi wake baada ya kusikia tetesi kuwa na uhusiano wa
karibu na mwanamuziki, Hamad Ally ‘Madee’. Kwa mujibu wa chanzo, mwanamuziki huyo
alikuwa akitokea kwenye mgahawa uitwayo Rapsody, ambapo alipofika maeneo
ya Salenda gari lingine lilipita mbele yake na kumziba ambapo mpenzi
wake huyo alishuka ndani ya gari na kumuomba ampe funguo.
Lulu Diva.
“Yaani ilikuwa ni aibu kwa Lulu, kwanza
mavazi aliyovaa hayaelezeki hata kidogo na mpenzi wake huyo aliomba
washuke wote kwenye gari huku akimwambia kuwa aendelee na Madee hivyo
amuachie gari lake,” kilisema chanzo. Star Mix lilimtafuta Lulu ili kuthibitisha madai hayo, ambapo alikiri kufikwa na masaibu hayo.
Lulu Diva na Madee.
“Unajua mambo mengine ni wivu tu wa
kimapenzi ni kweli alinifanyia hivyo kwa ajili ya Madee, wakati huyo ni
kama kaka yangu lakini nashukuru Mungu baada ya hali kutulia
amenirudishia gari,” alisema Lulu. Na Imelda Mtema.
Post a Comment